Mzee Msekwa
IKIWA zimebaki siku nane kabla ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kuadhimisha miaka 36 ya kuzaliwa kwake, makada wakongwe
wa chama hicho, Pius Msekwa na Ibrahim Kaduma wamesema ili kudumisha
umoja ni lazima wanachama wakorofi ndani ya chama hicho wachukuliwe
hatua.
Kauli za wanachama hao wakongwe zimekuja wakati
ambao watu wa kada mbalimbali wamekuwa wakikilalamikia chama hicho kwa
kushindwa kuwachukulia hatua baadhi ya makada wake, ambao wanatajwa
katika kashfa mbalimbali, huku wakidaiwa kukigawa chama hicho.
Sherehe hizo za CCM zinazofanyika kitaifa mkoani
Kigoma zitafikia kilele chake Februari 3, mwaka huu, huku kikipanga
kuzitumia sherehe hizo kufanya tathmini ya uchaguzi wake mkuu
uliomalizika mwishoni mwa mwaka jana.
Kwa nyakati tofauti Msekwa ambaye amewahi kuwa
Kaimu Mwenyekiti wa CCM, Bara na Kaduma aliyewahi kuwa Waziri katika
Serikali ya Awamu ya Kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere, walisema uadilifu
ndiyo kitu cha kwanza kuzingatiwa ndani ya chama na taifa kwa jumla.
Msekwa alisema kuwa watu wakorofi ndani ya CCM
hawawezi kukosekana kwa kuwa chama ni jumuiko la watu wengi na kwamba
kila mmoja ana tabia zake.
“Hiyo ndiyo hali halisi, hata ndani ya nchi
yetu kuna watu wabaya na wazuri na ndiyo maana zikawapo sheria kwa
ajili ya kuwashughulikia wanaozivunja,” alisema Msekwa na kuongeza:
“Hata CCM ina kanuni na taratibu zake za kuwashughulikia watu wanaokwenda kinyume na taratibu za chama.”
Alisema kuwa chama hicho kimeweza kumitimza miaka 36 kwa ajili tu ya kufuata misingi iliyoachwa na Mwalimu Julius Nyerere.
“Hata waliopo sasa, nao wanafuata misingi hiyo na
ndiyo maana unaiona CCM ipo hapa, ila kikubwa ambacho chama imekifanya
ni kujali shida za watu,” alisema Msekwa.
Alifafanua: “Watanzania wanaona ni bora waongozwe
na CCM kwa sababu hawajawahi kutawaliwa na chama kingine, ambacho labda
wangekilinganisha utendaji wake na huu wa CCM, hivyo wanaona bora kubaki
na CCM.
Kwa upande wake Kaduma ambaye katikati ya wiki hii
alitoa maoni yake ya Katiba Mpya, alisisitiza kuwa alichokizungumza
katika maoni yake, ndiyo kasoro za CCM.
Alisema upungufu ulio ndani ya CCM ni maaadili ya viongozi wa kada mbalimbali.
Alisema kuwa ili kumaliza suala la uadilifu, taifa linatakiwa
liwe na tume huru ya maadili, ambayo itakuwa juu ya viongozi wote ikiwa
ni pamoja na rais.
Alipendekeza tume hiyo iundwe na Watanzania
kubainisha misingi na maadili ya taifa, pamoja na wajumbe wake
kupatikana kwa kuwashirikisha wananchi, ambao ndiyo watapendekeza majina
ya watu watakaokuwa viongozi wa tume hiyo.
Alisema kazi ya tume hiyo itakuwa kuchunguza
mienendo wa viongozi wakuu wa mihimili muhimu ya uongozi wa taifa kama
Rais, Makamu wake, Spika wa Bunge, Majaji, Mawaziri, wabunge na viongozi
wa vyombo vya ulinzi na usalama.
“Kazi nyingine ya tume hii itakuwa ni kutoa mapendekezo kwa Bunge kuhusu uadilifu wa Rais katika kutekeleza majukumu yake,
No comments:
Post a Comment