MTUHUMIWA WA KESI YA WIZI WA SHILINGI MILIONI 15.6 MALI YA SERIKALI YA WANAFUNZI UDOM KITIVO CHA SAYANSI YA JAMII SANAA NA LUGHA IDDY MOHAMMED NA WENZAKE WAACHILIWA KWA DHAMANA


Aliyekuwa Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha Idd Mohammed (Wa Sita kutoka Kulia Waliokaa Kwenye Viti) Alipokuwa Kwenye moja ya Kampeni zake za Kuwania Kiti Cha Uraisi Mwaka Jana Chuoni Hapo

Aliyekuwa Raisi Wa Kitivo Cha Sayansi ya Jamii,Sanaa na Lugha Cha Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)  ambaye pia ni Mwanafunzi wa Mwaka wa 3 wa Kozi ya Biashara na Akaunti (BCOM Accounting) Idd Mohammed mnamo alhamisi alishikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Dodoma katika Kituo Cha Polisi Cha UDOM kwa tuhuma za Wizi wa Pesa Za Kitanzania Shilingi Milioni 15.6 mali ya serikali ya wanafunzi wa kitivo hiko ambazo aliweza kuhamisha kutoka Kwenye Akaunti ya Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo Hiko Kwenda kwenye Akaunti Binafsi ya Waziri Wa Fedha Wa Kitivo Hiko Ibrahim Matata.


Raisi huyo pamoja na Waziri wake wa fedha walikamatwa jana alhamisi na Polisi huku wakikutwa na Pesa taslimu shilingi Milioni 7,224,000 ambazo walikutwa nazo mikononi. Chanzo chetu kilienda kusema kuwa Awali Raisi huyo inasemekana aliwaweka watia saini anaowataka yeye kinyume na taratibu na kuwatoa waliowekwa kwa taratibu na Sheria za Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo hiko kuwa ndio watu wenye dhamana ya kuruhusu pesa za Serikali ya Wanafunzi kutoka Katika Akaunti hiyo ya Serikali ya Wanafunzi.

Chanzo Chetu kiliendelea Kutupasha kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri wake wa Fedha walikamatwa Jana na kulala katika Kituo Cha Polisi Cha UDOM tayari kwa Uchunguzi na hatua za kisheria Kuchukuliwa dhidi yao.

Habari zaidi ambazo HABARI NA MATUKIO  imezipata kutoka katika Vyanzo tofauti tofauti Zinadai kuwa Raisi huyo pamoja na Waziri wake Wa fedha wanaweza kufikishwa Mahakamani Jumatatu kwaajili ya kusomewa mashtaka yao ikiwemo tuhuma za wizi wa Shilingi Milioni 15.6 ambazo walikutwa nazo mkononi na kiasi kingine kubaki kwenye akaunti Binafsi ya Waziri Huyo wa Fedha Ibrahim Matata 

Baada ya Bunge la Serikali ya Wanafunzi wa Kitivo Hiko Cha Sayansi ya Jamii, Sanaa na Lugha kukaa jana Majira ya Saa Kumi Jioni nakuweza Kutoa uamuzi wa Kumvua Madaraka Raisi huyo ambapo imepelekea Baraza zima la Mawaziri kuvunjwa na kupelekea Spika Wa Bunge Kushikilia Serikali Hiyo Kwa Muda.

"Kwenye Majira ya Saa 10 jioni ya leo (Jana) bunge lilikaa na ndipo Spika alipoamua kuchukua uamuzi uliotolewa na wabunge wa kumvua madaraka raisi huyo na kupelekea Baraza la mawaziri kuvunjwa na Serikali kushikiliwa na Spika Wa Bunge hilo" Kilisema Chanzo Chetu.


Kwenye Majira ya Saa Moja Jioni ya jana aliyekuwa raisi wa Kitivo Hiko Idd Mohammed na aliyekuwa waziri wa fedha Ibrahim Matata Waliweza kuachiwa kwa Dhamana na Sasa Wapo Nje Kwa Dhamana


Chanzo Chetu kiliendelea kudai kuwa Kuna fununu zilizozagaa kwa baadhi ya wanafunzi wachache wa kitivo hiko Kuwa Inasemekana Aliyekuwa Raisi Wa Kitivo Hiko ana kashfa ya Kuomba Rushwa ya Shilingi Milioni Moja laki moja na hamsini elfu ( 1,150,000 ) katika Duka lililopo bweni namba 13 (block 13) ambapo chanzo hiko kimedai kuwa kulikuwa na ushahidi wa Sauti ambao ulirekodiwa wakati Mtuhumiwa huyo akiomba rushwa kabla ya kukamatwa hapo juzi kwa tuhuma za Wizi wa Shilingi Milioni 15.6 akiwa na aliyekuwa waziri wake wa fedha Ibrahim Matata.

No comments:

Post a Comment