Mama
Vailet Nyamanga (41) akiwa na Mtoto wake Rose Nyamanga (9) wakikatiza
katikati ya mitaa ya Nkuhungu Wilaya ya Dodoma Mjini katika Mkoa wa
Dodoma, hivi karibuni. Rose ni mwanafunzi wa darasa la pili katika shule
msingi Nkuhugu, Mama huyu, Vailet, ambaye ni mremavu wa viungo mwenye
urefu wa futi mbili, Anaishi kwa kutegemea msaada kutoka kwa
wasambaliwema ambapo kwa siku anaweza kujipatia sh. 2000 hadi sh. 4000.
Na
mwanawe Rose ndiye hasa msaada mkubwa kwa mama yake ambaye humuongoza
pindi wanapokuwa barabarani katika safari zao za kutafuta riziki na pia
ndiye humuhudumia mama yake kwa kumsafisha pindi anapokuwa amejisaidia
na pia humlisha chakula na kumuogesha na kumvarisha nguo.
Rose alianza kumhudumia mama yaketangu akiwa na umri wa miaka (5).
Mama
huyo hadi sasa ana watoto wawili Rose akiwa ni wapili kuzaliwa wa
kwanza ni wa kiume ambaye ana umri wa miaka (19), anayeitwa Cristopher
Nyamanga, ambapo watoto wote alijifungua kwa kufanyiwa upasuaji katika
Hospitali ya Mkoa wa Dodoma, lakini hadi sasa baba wa watoto hao
hawajulikani walipo baada ya kumkimbia baada ya kupata ujauzito.
Na
Mkubaru Blog
No comments:
Post a Comment