Mwanafunzi Chuo Kikuu cha Saint John auawa kinyama.
Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime
Polisi
mkoani Dodoma imeshutumiwa kwa kushindwa kuimarisha ulinzi katika
baadhi ya maeneo mkoani humo hatua inayodaiwa kuchangia kuaawa kinyama
kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Saint John Lidya Leo Mzima na watu
wasiojulikana.
Marehemu Lidya mwenye umri wa miaka 57 anadaiwa kuuawa siku ya
jumapili majira ya saa nne za usiku pembezoni mwa maeneo ya chuo hicho
chenye wanafunzi 5500 akiwa anarejea nyumbani baada ya masomo ya jioni.
Ni simanzi, vilio, huzuni na majonzi katika vyunga vya chuo hiki
kufuatia tukio hili la kusikitisha ambalo linadaiwa kuyaweka katika
mashaka na wasiwasi mkubwa maisha ya wanafunzi hawa.
Licha ya kulitupia lawama jeshi la polisi baadhi ya mashuhuda walidai
kuwa baada ya kufikwa na mkasa huo uliositisha safari ya maisha yake
mwili wa marehemu Lidya uliharibiwa vibaya na mnyama asiyejulikana kwa
kunyofolewa macho, masikio, pua, mguu na viuno vingine.
Kutokana na shutuma za uzembe dhidi ya jeshi hilo Kamanda wa mkoa wa
Dodo,a Kamishna msaidizi wa Polisi David Misime aliwataka wakazi wa mkoa
huo kuimarisha ulinzi shirikishi kwa lengo la kuwabaini wahalifu.
Wakati huo huo Kamanda Misime alisema msako mkali umeanza wa kuwatia
nguvuni waliohusika na ukatili huo ili waweze kufikishwa kwenye mikono
ya sheria kwa ajili ya hukumu.
Wanafunzi wa Chuo Cha Saint John walikuwa wakiripotiwa kukumbwa na
vitendo vya kubakwa, kulawitiwa, kuporwa mali zao sanjari na kupewa
vipigo na watu wasiojulikana pasipo sababu za msingi.
Mwili wa marehemu Lidya aliyekuwa muuguzi kitaaluma umehifadhiwa
kwenye chumba cha maiti katika hospitali kuu ya Mkoa wa Dodoma ukisubiri
uchunguzi wa madaktari.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amina.
No comments:
Post a Comment