Baraza la Usalama la Umoja wa
Mataiafa limetoa wito kwa kundi la wapiganaji katika Jamhuri ya Afrika
ya Kati wasiingie mji mkuu, Bangui, na watoke katika miji waliyoiteka.
Baraza la Usalama limewataka wapiganaji hao washiriki katika mazungumzo ya amani yatayoanza nchini Gabon juma lijalo.
Wapiganaji hao ambao walikaribia mji mkuu wa
Bangui hivi karibuni wanataka rais wa jamhuri hiyo ya Afrika ya Kati,
Francois Bozize, ajiuzulu.
Jamhuri ya afrika ya Kati ni moja kati ya nchi maskini kabisa barani Afrika na imepita kwenye mizozo mingi.
No comments:
Post a Comment