Afrika Kusini imethibitisha
kwamba imetuma wanajeshi zaidi huko Jamhuri ya Afrika ya Kati huku
wapiganaji wanaendelea kusonga dhidi ya serikali.
Msemaji wa wizara ya mashauri ya nchi za nje
mjini Pretoria alieleza kuwa wanajeshi 120 zaidi wametumwa kulinda
wanajeshi wa Afrika Kusini ambao tayari wako Jamhuri ya Afrika ya Kati
kulifunza jeshi la serikali.
Ofisi ya Rais Zuma inasema kuwa serikali imeidhinisha jumla ya wanajeshi 400 kutumwa huko.
Wapiganaji na serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wanatarajiwa kuanza mazungumzo katika siku za karibuni.
No comments:
Post a Comment