SPIKA wa Bunge, Anne Makinda
SPIKA wa Bunge, Anne Makinda amesema hoja zote
binafsi zilizositishwa katika Bunge la 10, sasa zitajadiliwa katika
Bunge lijalo litakaloanza Aprili 9. Makinda alisema wahusika wa hoja,
wanatakiwa kujipanga upya na kuwasilisha hoja zao.
Makinda kwa sasa anahudhuria Mkutano wa
Halmashauri Kuu ya CCM Dodoma. Hata hivyo, ni hoja pekee ya Joshua
Nassari kuhusu mwenendo wa Baraza la Mtihani la Taifa (Necta)
unavyoathiri elimu ya Tanzania ndiyo haikusomwa kutokana na kuzuka kwa
vurugu katika mkutano huo wa Bunge.
Hoja binafsi ziliwasilishwa ni ya Mwigulu
Nchemba iliyokuwa ikihusu mikopo ya elimu ya juu, James Mbatia iliyohusu
mitalaa ya elimu kwa shule za msingi, sekondari na elimu ya awali.
Hamisi
Kigwangala aliwasilisha hoja yake ya kuanzishwa mpango wa kusaidia
vijana ikiwamo kuanzisha benki,wakati John Mnyika aliwasilisha hoja
kuhusu maji na majitaka katika Jiji la Dar es Salaam.
Hata hivyo, hoja za Kigwangala na Nchemba
ndizo zilizopita wakati hoja ya Mbatia na Mnyika zilitupwa baada ya
mijadala ya hapa na pale kwa wabunge.
Kwa upande mwingine, hoja za Mbatia na Mnyika
ndizo zilizowasha moto Bungeni na hata kusababisha Kamati ya Maadili,
Haki na Madaraka ya Bunge kuamua kuondoa hoja zote kutokana na vurugu
hizo ambazo Spika alisema sehemu kubwa zimesababishwa na Mbunge wa
Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.
Makinda alisema pia kuwa pamoja na kuahirisha
Bunge, lakini wabunge wametia aibu kubwa ndani ya taasisi hiyo ambayo ni
moja ya mihimili ya dola.
No comments:
Post a Comment