KIONGOZI Mkuu wa madhehebu ya Othodox Afrika, Papa Beatitude Theodoros II anatarajia kukutana na Rais Jakaya Kikwete.
Kiongozi huyo aliyewasili nchini jana, alisema
anatarajia kukutana na Rais Kikwete kesho na miongoni mwa mazungumzo yao
ni jinsi ya kanisa hilo litawaletea maendeleo Watanzania.
“Nitazungumza naye juu ya mipango niliyonayo ya maendeleo Tanzania na kuomba ushirikiano zaidi,” alisema Papa Theodoros II.
Alisema Kanisa la Othodox limekuwa likiendesha
miradi mbalimbali kusaidia Watanzania ikiwapo hospitali itakayogharimu
Sh17 bilioni, inayojengwa Nyegenzi, mkoani Mwanza.
Miradi mingine ambayo kanisa hilo linatarajia
kuanzisha nchini ni kujenga vituo vya watoto yatima, vituo vya ushauri
na kutoa matibabu kwa waathirika wa virusi vya Ukimwi (VVU) na ujenzi wa
shule.
“Nina mpango wa kukutana pia na Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, ili kuweka mikakakti jinsi ya kuendeleza elimu
nchini,” alisema Papa Theodoros II.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Othodox, Jimbo Kuu la
Mwanza, Jeronmos Muzeyi alisema ujio wa Papa Theodoros II nchini ni
kuandika historia ya pekee kwa sababu ni mara ya kwanza.
Alisema Papa huyo amefurahia mazingira na ukarimu
wa Watanzania na kwamba, atakuwa akifanya ziara za mara kwa mara ikiwa
ni sehemu ya kuzidi kujenga uhusiano.
Alisema lengo kuu la kanisa hilo ni kuendeleza
amani, upendo na mshikamano kwa Watanzania wote na kuhakikisha wanapiga
hatua zaidi za maendeleo.
No comments:
Post a Comment