Askari wa Polisi akiangalia zoezi la uteketezaji wa Silaha haramu
uliozinduliwa na Makamu wa Rais Dk Mohammed Ghalib Bilal uliofanyika
Ukonga jijini Dar es Salaam jana.Picha na Venance Nestory
ZAIDI ya silaha haramu 3,100 zimeteketezwa ili kukabiliana na uhalifu unaokumba nchi za Afrika Mashariki.
Akizungumza kwenye mkakati huo kuangamiza silaha
hizo Dar es Salaam jana, Makamu wa Rais, Dk Mohammed Gharib Bilal
alisema bado kuna kazi kubwa kukabiliana na migogoro eneo hilo
kutokana na wimbi la umiliki wa silaha haramu.
Silaha hizo ziliteketezwa kwenye viwanja vya Magereza Ukonga, huku viongozi mbalimbali wa kitaifa na kimataifa wakihudhuria.
Dk Bilal alisema migogoro mbalimbali na usugu wa
matukio ya uhalifu katika jamii, yanachangiwa na uwapo wa silaha ndogo
na kubwa ambazo zinazomilikiwa kinyume cha sheria.
Alibainisha kuwa takwimu zinaonyesha kuna sillaha
500,000 ukanda wa nchi za Afrika Mashariki zinamilikiwa na watu wa
aina mbalimbali kinyume cha sheria, jambo ambalo linasababisha
kuongezeka kwa matukio tofauti hasa maeneo ya mipakani.
No comments:
Post a Comment