Mwanafunzi ajimwagia,anywa mafuta ya taa, kujichoma moto na kufa
Waomblezaji wakiwa nyumbani kwa maruhemu
Wanafunzi wenzake wakiwa na masikitiko kwa kuondokewa na mwenzao
Na John Banda, Dodoma
Mwanafunzi wa kidato cha pili katika shule ya Sekondari Nzuguni
iliyopo manispaa ya Dodoma amekufa kwa kujichoma moto baada ya Mjomba
wake kumchapa viboko kutokana na kosa la kutomsaidia Bibi yake kuosha
vyombo.
Tukio la kifo cha mwanafunzi huyo lilitokea jana jumapili ambapo saa
11 jioni katika hospital Rufaa ya General Dodoma baada ya kulazwa kwa
masaa kadhaa.
Akisimulia kifo marehemu nyumbani kwa mwenyekiti wa mtaa wa maweni B. mjomba wa marehemu
Paul Samwel 21 alisema kuwa siku hiyo ya tukio alitoka kazini kwake
mapema akarudi nyumbani na kumkuta mama yake akiingia jikoni baada ya
kutoka kuosha vyombo ndipo alipotaka kujua alipo Catherine kwani siku hiyo ya ijumaa wanawahi kutoka shule.
Samwel alisema mama huyo alimjibu kuwa Katherine alipofika alitoka na hajui
alipoelekea ndipo alipomsubili mpaka aliporudi akamuuliza kwamba kwanini
alimuacha Bibi yake afanye kazi wakati anajua haoni vizuri ndipo akamua
kukata fimbo na kuanza kumchapa alipotosheka akamuacha baada ya muda
akiwa nyumba jirani alisikia kelele nyumbani.
''ndugu yangu nilikuta mjomba anaungua mwili mzima kuanzia kichwani
tuliposaidia na kumpeleka hospital mwili wote haukuwa na kazi bali moyo
tu ndiyo ulikuwa ukidunda pekee na jana jumapili saa 11 jioni alikata
roho kwa weli ameniuma sana maana ni kama mdogo wangu maana mama yake
alimuacha akiwa mdogo sana'', alisema Samwel
Kwa upande wa Wanafunzi wenzake waliofika kuomboleza nyumbani hapo walisema Marehemu alikuwa
akilalamika mara kwa mara kuwa alikuwa akiteseka sana nyumbani kiasi cha
kila siku kupewa adhabu za vipigo na mjomba wake huku akitaka fedha kwa
Babu yake za kunulia vifaa vya shule na mahitaji mengine kama mtoto wa
kike alikuwa anachapwa pia.
Wanafunzi hao Desleria Lupembe, Elika Zabron, Maria Paul na Anastadhia
Boniface Wote wa kidato cha pili Nzuguni walisema kwa siku zilivyokuwa
zinazidi kusogea karibu na kifo chake walikuwa wakimshangaa mwenzao
huyo.
''Mara kwa mara alikuwa akituambia wakati wowote atakufa hivyo tumpe
picha zetu ili awe anatuangalia na sisi hapa unayetuona tulishampa zetu,
lakini alhamis akawa serios sana akasema mambo yamezidi hata jumatatu
hatakuja shule na hatutaonana kwasababu siku hiyo alinyimwa hela na Babu
yake mzee Samwel pamoja na kuchapwa sana huku akiambiwa amfuate mama
yake'', alisema Maria paul [15]
Nae Bibi wa marehemu Juliana
Samwel akizungumzia tukio hilo alisema baada ya kuchapwa na mjomba wake
Kathe alichukua mafuta ya taa na kujimwagia mwili mzima na mengine
akayanywa kisha akijiwasha na njiti ya kiberiti akawaka mwili mzima
kiasi cha yeye kushindwa kumsaidia.
mwanangu mtoto aliungua karibu mwili mzima maana alikuwa
amejiviringisha kanga toka chini mpaka juu nilipiga kelele majirani
wakaja kuzima ule moto na kumbe alishaungua sana hata ngozi ilikuwa
ikijichubua yenyewe, mzee Samwel angekueleza mengi lakini kaenda
hospital kuuhifadhi mwili maana mama ya mrehema ndiyo leo anatoka Dar
hivyo mazishi ni kesho mapema, kuhusu kifo sina cha kufanya imetokea
imetokea nitafanyeje'', alisema. mama huyo wa umri kati ya 50/55
Kwa upande wa majirani walisema tukio hilo lilikuwa la kutisha na si
la kawaida kuwahi kutokea imeonyesha watoto wa sasa siyo wa kunyanyaswa
hovyo, wakatoa ushauri kuwa kila mwenye mtoto akae na mwanae asimuamini
mtu ndiyo sababu ya watoto wengi hasa wa kike kuharibikawa kutokana na
kukosa uangalizi.
MWISHO
No comments:
Post a Comment