Eneo la Kaskazini mwa Kenya limekumbwa na vmashambulizi ya mara kwa mara yanayofanywa na Al Shabaab
Watu saba
wameuawa kwa kupigwa risasi katika shambulizi karibu na msikiti
Kaskazini Mashariki mwa Kenya, karibu na mpaka na Somalia.
Wanakijiji waliambia BBC kuwa watu kumi
waliokuwa wamejihami waliwashambulia kwa bunduki watu hao wakati
walipokuwa wanaondoka msikitini mapema asubuhi.
Mwanzo wanaume watano waliuawa na kisha wanawake wawili waliosikia milio ya risasi walipofika kuchunguza, nao pia wakauawa.
Shambulio linafanyika chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi kufanyika katika eneo mojawapo ambapo usalama ni tatizo kubwa.
Wenyeji wa kijiji cha Malaley wanasema kuwa hakuna kilichoibiwa kwani washambuliaji walitoroka punde baada ya shambulizi.
Kijiji hicho kiko umbali wa kilomita 45 kutoka
kambi ya wakimbizi ya Dadaab ambayo ni makao kwa wakimbizi zaidi ya laki
tano, waliotoroka vita nchini Somalia.
Katika mwaka mmoja uliopita, eneo hilo
limekumbwa na mashambulizi ambayo yamelaumiwa kwa kundi la wapiganaji wa
kiisilamu Al Shabaab.
Al-Shabab iliahidi kulipiza kisasi wakati
wanajeshi wa Kenya walipokwenda Somalia kupambana nao, mwezi Oktoba
mwaka 2011 kama juhudi za kusaidia wanajeshi wa muungano wa Afrika.
No comments:
Post a Comment