KAMPUNI ya Star Media imeanzisha huduma mpya ya
kukodisha ving’amuzi kwa wateja wao, ili kujipatia matangazo ya
televisheni kwa mfumo wa dijitali ambao ulianza kutumika rasmi mwanzoni
mwa mwaka huu.
Ving’amuzi hivyo vilivyoanza kutolewa jana kwa mkopo, vinawalenga watu wote ambao wako tayari kunufaika na fursa hiyo.
Viitakuwa na chaneli 15 zikiwamo za Tanzania na nyingine zitazoongezwa.
Meneja
Masoko wa Star Times, David Kisaka alisema masharti ya kupata huduma
hiyo ni mteja kulipia Sh39,000 kama dhamana ya king’amuzi, Sh6,000 ikiwa
ni kukodisha.
“Hii ni promosheni ya mwaka mmoja hadi mitano,
muda utaanza kuhesabiwa rasmi mteja atakaposaini mkataba wa makubaliano
na Star Times. Pia, mteja anaweza kuongeza mkataba wa ukodishaji hata
baada ya miaka mitano kumalizika,” alisema Kisaka.
Alisema ili kupata huduma hiyo kwa mara ya
kwanza, mteja anatakiwa kusoma, kuelewa na kujaza fomu ya makubaliano
ambayo yamefuata sheria na haki zote kulingana na Katiba ya Tanzania.
Kisaka alisema Star Times wakishirikiana na
TBC na Star Communication Technology wamejipanga kikamilifu kusambaza
huduma za dijitali maeneo mbalimbali nchini kwa gharama nafuu.
No comments:
Post a Comment