Na John Banda,Dodoma
VIZIWI
wanaoishi vijijini wa mji mdogo wa Kibaingwa Wilaya ya Kongwa wale
wanaoishi vijijini ,wamesema watashindwa kuchangia mawazo yao ya
marekebisho ya katiba mpya inayoendelea kwa hivi sasa kwa kuwa
hawajawahi kukiona kitabu cha katiba na pia hawajawahi kukisoma bali
wanasikia kupitia kwenye vyombo vya habari ikitanganzwa.
Kauli
hiyo
imetolewa kwa pamoja na walemavu Tito Mnyamale (33) na Paul Mnage (32)
kwa niaba ya wezao wakati wanapokuwa wakichangia juu ya marekebisho
yanayotakiwa yafanyike kuhusu haki zinazotakiwa kutendewa watu wenye
ulemavu wa
kutosikia.
Wakichangia hoja zao kwenye warsha ya mafunzo
ya mkataba wa umoja wa mataifa juu ya haki ya walemavu na sheria na sera
ya Taifa ya viziwi mwaka 2010 kwa viziwi wa mji wa mamlaka ya Kibaingwa
Wilaya ya Kongwa.
Walemavu
hao walisema wanashindwa kuchangia katiba hiyo kutokana na kutoielewa
na itawasaidiaje wao wakati toka wamezaliwa hawajawahi kuiona na badala
yake wanaisikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari.
"Hapa lazima
tuiambie ukweli serikali yetu kuwa sisi walemavu tunaoishi vijijini
hatujakiona hiki kitabu ambacho leo hii tunaambiwa ndiyo katiba
inayotakiwa kufanyiwa marekebisho mbalimbali,hii pia inatokana na kwa
upande wetu kukosa kushirikishwa kwenye vikao vinavyozungumzia
marekebisho hayo ya katiba"alisema Mnange.
Aidha walemavu hao walisema kutokana na viongozi wa serikali ngazi
ya kata,vijiji hadi vitongoji kitendo chao cha kutowashirikisha kwenye
vikao vya kujadili katiba hiyo pia kumechangia kwa upande wao kutoipata
elimu ya kutosha ambayo ingetuwezesha kufahamu namna ya kuijadiri
marekebisho hayo.
"Serikali yetu kwa kupitia viongozi wao wamekuwa wakiwaona wa maana
sana katika kipindi cha upigaji kura tu,na wako radhi kuja kutubeba
kwa usafiri wao ili waweze kupigiwa kura za kuwachangua lakini kwenye
suala la kujadili mapendekezo ya marekebisho ya katiba inaonekana sisi
haituhusu kabisa"alisema Tito.
Naye Meneja wa mradi wa Leonard
Cheshine Disibility Dodoma Baraka Mgohamwende aliwataka walemavu hao
kutoa maoni yao juu ya haki wanazotaka zifanyiwe kwa kupitia katiba hiyo
mpya ambayo hivi sasa inajadiliwa na kupendekezwa na watanzania hapa
nchini.
Mgohamwendo ambaye alikuwa akielimisha umuhimu wa kuitambua
katiba kwenye warsha hiyo, alisema kuwa pamoja na kutoielewa maana ya
katiba hiyo ambayo hivi sasa wameiona na kukabidhiwa,wanatakiwa kuisoma
ili kupitisha maoni yao ambayo yanayohitajika kuwepo na haki zao
zinazotakiwa waweze kufanikisha.
Naye Katibu wa Chavita wilaya ya Kongwa Anitha Masawe alisema katika
eneo hilo walemavu wa Uziwi walio wengi hawaitambui katiba hiyo
inatokana viongozi walio kwenye ngazi za vitongoji,vijiji na kata kwa
upande wa serikali na
siasa hawaoni umuhimu wa kuwashirikisha shughuli mbalimbali za
kimaendeleo.
Anitha alisema ndiyo maana leo hii walemavu wa
wilaya hiyo hususan wale wanaoishi vijijini,hawajui katiba na faida
ambazo watakazoziona kama na wao watachangia katika kutoa mapendekezo ya
marekebisho ya katiba hiyo.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment