Shamba la mpunga
BAADHI ya wakulima wa zao la mpunga Wilaya ya
Mbarali, Mkoa wa Mbeya wameiomba Serikali kuwafikishia wataalam wa
kilimo, ili waweze kuwapatia elimu ya kilimo bora cha kisasa ili
kuongeza kasi ya uzalishaji wa zao hili na kupata soko la uhakika la
ndani na nje kwa kutumia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Songwe.
Wakizungumza na gazeti hili jana katika
kata ya Igurusi,walisema elewa mdogo wa kutozingatia kanuni bora za
kilimo ni chanzo cha kutopata mazao mengi ya chakula na biashara hususan
ukosefu wa dhana za kisasa za kilimo,ambapo baadhi yao bado wanaendelea
kutumia kilimo cha ng’ombe na punda.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima,Amos
Matanana alisema uelewa mdogo wa kuzingatia kanuni bora za kilimo ni
chachu kwao na kwamba ni wakati wa serikali sasa kuwasaidia wakulima
vijijini kufikiwa na wataalamu wa kilimo ili waweze kupatiwa elimu
kupanda mazao kwa kuzingatia utaalam wa kilimo bora na cha kisasa.
Aidha alisema kuwa wakulima wamekuwa
wakikumbwa na changamoto nyingi hususan kipindi cha msimu wa kilimo,
ukosefu wa skimu za umwagiliaji na kwamba hali hiyo imekuwa ikichangia
wakulima kutopata mazao mengi katika msimu wa mavuno.
Alisema wanaiomba serikali kuangalia uwezekano
wa kuwafikishia mikopo ya matrekta madogo (powertiller) ili waweze
kuzalisha zao hilo kwa wingi na kupata soko la uhakika litakaloweza
kumkwamua kiuchumi mkulima mmoja mmoja kiuchumi.
No comments:
Post a Comment