WAKAZI wa Kata ya Nyamongo mkoani Geita
wamewalalamikia viongozi wa Chadema kwa kushindwa kujenga barabara
,shule na zahanati katika Kijiji cha Ilyamchele, Kata ya Nyamongo mkoani
Geita kama ilivyowaahidi.
Walisema tangu uchaguzi wa mwaka 2010, mpaka
sasa kata yao haijafanya maendeleo yoyote na kwamba ahadi zilizotolewa
hazijatekelezwa mpaka sasa.
Lawama hizo zilikuja baada ya wananchi wa
kijiji hicho kutoa kero zao katika mkutano wa hazara uliandaliwa na
UVCCM mkoa ,ambapo wananchi hao walisema Chadema ilipoingia madarakani
iliahidi kutengeneza barabara ,shule na zahanati lakini mpaka leo hata
mbunge aliyechaguliwa wala diwani hajawahi kukanyaga katika kijiji
hicho.
Wakijibu hoja hizo viongozi wa UVCCM walisema
hayo ndiyo matunda ya chama makini walichokichagua,na kusema Chadema
wasitumie siasa kudanganya wananchi, na kwamba Chadema haina nia njema
na wananchi bali ni uchu tu wa kutaka madaraka.
“Mnaona sasa waliwaahidi watawaletea barabara
iko wapi hata sisi wakati tunakuja huku tumechelewa kufika kwasababu ya
barabara mbovu imejaa visiki na makorongo halafu mnajiita mna kiongozi
bora “alisema Katibu wa UVCCM Mkoa wa Geita, Jonathan Mabihya.
Mabihya alisema kuwa,Chadema walionyesha kuwa
wao ni bora zaidi ya chama kilichopo madarakani na CCM ikaamua
kuwaruhusu walau wachukue baadhi ya majimbo ili kuona kama kweli wao
wanaweza kuongoza nchi, lakini kwa kipindi kifupi tu viongozi hao hao
wanaiba fedha za umma ,wanashindwa kutekeleza yale waliyowaahidi
wananchi.
“Naomba niwaeleze wananchi wa Ilyamchele
huenda mlichagua Chadema kwa kutokujua,mkichagua CCM mtakuwa na uhakika
wa maendeleo kuliko Chadema niulizeni kwanini”alihoji Mabihya.
Aliongeza kuwa Chadema haiwezi kujenga
barabara,shule wala zahanati katika kijiji chicho kwasababu haina uwezo
huo, Awali wananchi waliokuwa katika mkutano huo walisema kijiji hakina
shule ya msingi na shule iliyopo ni ya awali ambayo imejengwa kwa
udongo.
No comments:
Post a Comment