Takriban asilimia tisini ya wanwake katika kijji kimoja inasemekana wameondolewa mfuko wao wa uzazi
Wakereketwa wa haki za kibinadamu wanasema kuwa maelfu ya wanawake wamekuwa wakiondolewa mfuko wa uzazi kwa ulaghai ambapo wanadanganywa kuwa watashikwa na saratani iwapo hawafanyiwi hivyo katika kliniki za kibinafsi.
Ifuatayo ni taarifa ya Jill Mcgivering ikisimuliwa na Wanyama wa Chebusiri.
Kuongezeka kwa visa vya wanawake kuondolewa mfuko wa uzazi, ni kutokana na ongezeko la kliniki na hospitali za kibinafsi katika miaka ya hivi karibuni.
Zote hizo zinajaza pengo la mfumo duni wa serikali hususan katika maeneo ya vijijini.
Wanaharakati wanataka hospitali hizo kuchunguzwa na hata kuwekewa sheria za utenda kazi ili kuhakikisha kuwa haziwanyanyasi akina mama maskini.
Daktari Narendra Gupta anayefanya kazi katika shirika moja lisilo la kiserikali, Prayas anasema kuwa madaktari wa kibinafsi, wameona fursa ya kutengeza pesa kwa haraka.
Anaelezea kuwa kuna mbinu nyingi tu ambazo, mfuko wa uzazi unaweza kuondolewa bila upasuaji, na kwamba hiyo inapaswa kuwa tu njia ya mwisho katika matibabu yoyote.
Mmjoa wa wanawake walioondolewa mfuko wao wa uzazi
No comments:
Post a Comment