TBL YATOA MSAADA WA 50MIL ZASAIDIE KUCHIMBA VISIMA
Na John Banda, Dodoma
Kampuni ya
Bia Tanzania [TBL] Imetoa msaada wa visima vilefu viwili vya maji kwaajili ya vijiji
viwili vya Iramba na Lukole vilivyopo wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma baada ya
kugundua upungufu wa maji uliopo katika vijiji hivyo.
TBL walitoa
msaada huo wa million 50 kwa ajili ya visima 2 baada ya kuombwa na mbunge wa
jimbo la kibakwe Mhe George Simbachawene baada ya kuona tatizo la ukosefu wa
maji kuwa kelo kwa wananchi wake.
Akiongea
baada ya kukabidhi hundi ya kiasi hicho cha Fedha Mkurugenzi wa Uhusiano na
Sheria wa kampuni hiyo Stiev Kilindo
aliwataka wanachi hao kuutunza mradi huo
ili uweze kuwa endelevu na kuja kuwa na manufaa hata kwa vizazi vijavyo.
‘’Tumetoa
visima hivi viwili ili maji yake yaweze kusaidia wakazi wa vijiji husika
niwashauri muweze kuitunza miradi hii ili iwe endelevu na kuwa sadia watoto na
wajukuu wetu muipende na kuirinda huku mkitunza mazingira wenye’’, alisema
Kilindo
Akizungumzia
tatizo hilo Mkuu wa wilaya hiyo Christofa Kangoye alisema
Chanzo cha tatizo hilo ni uharibifu wa mazingira unaotokana na kufyeka miti na
kulima katika vyanzo vya maji na
kutangaza kiama kwa watendaji.
Kangoye
aliwataka Maafisa watendaji wa kata kuhakikisha wanawakamata na kuwafikisha
kwenye vyombo vya sheria watu wote watakaobainika kujihusisha na uhalibifu wa
mazingira ikiwemo kufyeka, kulima na kupitisha mifugo kwenye eneo la Chemichemi
za maji.
‘’Watendaji
hakikisheni mnawachukulia hatua hata kama mnachukua hela zao maana mnahongwa
ndiyo maana mnajifanya hamuwaoni wanapokuwa wakiharibu mazingira iweje mpaka
tuje toka wilayani ndipo tujue uhalibifu huu ulioleta mazara kwa muda mrefu
sasa naanza na nyinyi’’, alisema Kangoye.
No comments:
Post a Comment