Na John Banda, Dodoma
POLISI
Mkoani Dodoma inawashikilia watu watatu baada ya kuwakuta wakiwa na
nyaya za Transfoma za jumla ya 20 milion mali ya Tanesco.
Nyaya hizo aina ya kopa
zenye uzito wa kilo 76 na nusu zilikutwa kwa watu hao baada ya msako wa
polisi wakishirikiana na Shirika la umeme Tanzania Tanesco
Kamanda
wa polisi mkoa wa Dodoma David Misime alisema nyaya hizo za matumizi ya
Transfoma hutumika kwa kufanyia Winding na nyingine ni kwa ajili ya
kuzuia Radi [earthing] na kwamba imebainika ziliibiwa maeneo ya kizota
na Ihumwa baada ya transfoma zake kuangushwa.
Misime aliwataja
waliokamatwa kuwa ni Abdul Bakari 17 mkazi wa Chang'ombe, Stanel Shayo
26 muuza vyuma chakavu Nkuhungu na Peter Kessy 50 mkazi wa Area E
manispaa ya
Dodoma.
Aliongeza kuwa jeshi hilo linamsaka Jamal Said Sondo wa Chang'mbe Juu aliyekimbia ya mfanyakazi wake Abdul Bakari kukamatwa
Kamanda
huyo amewataka wote wanaojihusisha na biashara ya vyuma chakavu
wajiepushe na kununua nyaya na vifaa vingine vya Tanesco pamaja na vyuma
vyote viavyohusiana na miundo mbinu.
Wakati
huohuo Jeshi hilo linamshikilia Denis Sadala 38 mkazi wa Mazase
Wilayani Mpwapwa Kwa kumkuta akimiliki Gobore bila kibali, huku
likiendelea kumsaka Matagi Charles 33 mkazi wa kijiji hicho aliyekimbia
na kutelekza Gobore alilokuwa akimiliki kinyume na Sheria.
No comments:
Post a Comment