WAKATI kondomu feki zilizopigwa marufuku
Uingereza mwaka jana zikiwa katika mzunguko nchini Tanzania, kesi za
gonjwa la ngono hatari lisilotibika zimeongezeka kwa asilimia 25
Uingereza, huku wataalamu wakionya kwamba ugonjwa huo umekuwa sugu zaidi
katika tiba.
Zaidi ya kesi 21, 000 za maambukizi mapya zimedaiwa kutambulika kwa mwaka 2011/12.
Kondomu hizo feki aina ya Trojan na Durex zenye
vipele vipele ambazo mwishoni mwa mwaka jana serikali ya Uingereza
iliingia katika msako mkali kusaka mamilioni ya kondomu hizo bandia
zilizokuwa zikiuzwa nchini humo miezi 18 iliyopita.
Kirusi kinachoambukiza ugonjwa huo hatari
kimetajwa kuwa ni 'Neisseria' ambacho ni tofauti na vingine ambavyo mara
nyingi hutibiwa kwa dozi moja tu ya viuavijasumu (antibiotics) ambayo
angalau hufanya kazi kwa asilimia 95 kiufanisi.
Akizungumzia maendeleo ya utafiti wa kondomu hizo
nchini , Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Wiwango Tanzania(TBS),Leandri
Kinabo alisema shirika hilo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Ckula na
Dawa(TFDA) hivi sasa lipo katika mchakato wa kuhakikisha vipimo halisi
vya ubora wa bidhaa hizo vinaangaliwa.
"Hili suala ni nyeti na ni la kiafya na usalama
zaidi, hivyo tulikaa kikao na TFDA na tulikubaliana tufanye uchunguzi wa
kondom hizi, kwani ni kweli zipo sokoni lakini suala la ubora
linatakiwa kuangaliwa," alisema Kinabo.
Aliwataka Watanzania kuwa na subira ili waweze
kuchunguza bidhaa hizo kwa umakini zaidi na kwamba baada ya uchunguzi
watatoa majibu.
Baada ya gazeti hili kutaka kujua uhalali wa
bidhaa hizo sokoni, Kinabo alisema bidhaa zote zinazoingia bandarini
hupimwa, lakini kuna baadhi ya bidhaa ambazo huingizwa kwa njia zisizo
halali na mara nyingi huwa feki.
"Inetegemea na lebo ya bidhaa husika, kuna wakati
bidhaa inaweza kupimwa na kuonekana kuwa ni salama na kisha kuingizwa
sokoni, lakini baada ya muda zikaingia bidhaa feki zenye nembo hiyohiyo,
hivyo hilo ni suala la kusubiri vipimo kutoka TFDA," alisema Kinabo.
Tatizo hilo sugu Uingereza limesababishwa
kuanzishwa kwa kampeni mpya ya kukabiliana na tishio kubwa la kuongezeka
kwa kasi kwa magonjwa hayo nchini Uingereza na Wales ambayo yamedaiwa
kusambaa kwa wingi nchini humo na nchi zinazoendelea.
Wataalamu wa Afya wana matumaini mapya baada ya
kuanzishwa mpango mkakati wa kuzuia ugonjwa wa gono 'Gonorrhoea
Resistance Action Plan' ambayo itaongeza ufahamu wa ugonjwa huo.
Mpango huo ulioanzishwa na shirika la Ulinzi wa
Afya, utafuatilia tatizo hilo la kimataifa linaloongezeka kwa kasi tangu
kupungua miaka 10 iliyopita.
Tatizo hili limeanza kukua kwa kasi mwaka 2011, wagonjwa wengi
waliojitokeza wameugua zaidi ya mara tatu magonjwa ya ngono. Zaidi ya
theluthi ya kesi hizi ni za wanaume waliokuwa wakifanya mapenzi na
wanaume wenzao, kutoka karibu ya robo kwa mwaka 2010.
Profesa Cathy Ison kiongozi wa kampeni hiyo
anasema "idadi kubwa ya watu waliougua magonjwa haya wanatamka kuwa
walipata kutumia kondom ambazo hata hivyo baadaye zilitambulika kuwa ni
feki na kuzuiwa hapa nchini Uingereza.
"Bado hatuwezi kuwahakikishia watu kuwa
tunatarajia kupata suluhu ya gono hili hatari, hili bado ni tatizo kubwa
kwa afya ya umma na ni kwamba sasa limeanza kusambaa hata nchi
zinazoendelea," anasema Ison.
Nchini Uingereza na Wales, kuna hatari kubwa ya
kuendelea kwa maambukizi haya ambayo hata hivyo yameonekana kukua kwa
kasi kubwa licha ya wagonjwa wengi kudai kuwa hutumia mipira katika
tendo la kujamiiana.
Ingawaje kesi za kushindwa kutibu gono hilo
zimekuwa ni taarifa za kimataifa, Afisa Mganga Mkuu Uingereza, Profesa
Sally Davies, hivi karibuni aliishauri serikali kuongeza nguvu katika
dawa za Antibiotics kwa ajili ya dharura kwa wagonjwa watakaopatikana na
gonjwa hilo.
Prof esa Davies anasema "tumeona na kuwa na
wasiwasi mkubwa katika kesi za dawa sugu za magonjwa ya zinaa kwa muongo
uliopita, lakini kuna haja ya kutengeneza dawa hizo kwa ajili ya tatizo
hili, labda tutafanikiwa, lakini kazi ya ulinzi wa shirika la afya ni
muhimu katika kutafuta suluhu ya tatizo hili" anasema.
Mdhibiti wa dawa na bidhaa za afya nchini humo,
alidai kwamba mamilioni ya kondom hizo feki ziliingia nchini humo
zikitokea Mashariki ya Mbali na kwamba zimeshatumiwa na watu wengi tangu
kuingizwa nchini humo.
Kondom hizo zilidaiwa kutengenezwa kwa vifaa
rahisi visivyo na ubora ambavyo vinaweza kuongeza hatari kwa watumiaji
kwa kusambaza kwa kasi magonjwa ya zinaa, au kusababisha mimba
zisizohitajika, pamoja na kuharibu mikakati ya uzazi wa mpango.(Herrieth
Makwetta)
No comments:
Post a Comment