Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii,Dr Hussein Mwinyi.
SERIKALI imejiwekea lengo la kutahiri wanaume
milioni 2.8 ifikapo mwaka 2015, baada ya kufanikiwa kuwatahiri 287,055
kati ya mwaka 2010 na 2012.
Hayo yamebainishwa katika taarifa iliyotolewa na
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ikifafanua kuwa huduma ya tohara ya
kitabibu kwa wanaume ilianzishwa mwaka 2010.
Imetekelezwa zaidi mikoa ambayo ilibainika kuwa na kiwango cha juu cha maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
“Iligundulika kiwango cha juu cha maambukizi ya
VVU ambako kuna kiwango cha chini cha tohara kwa wanaume. Mikoa hiyo ni
ya Iringa, Njombe, Simiyu, Geita, Katavi, Mbeya, Rukwa, Tabora,
Kagera, Mwanza na Mara,” inaelezwa taarifa hiyo.
Inaelezwa kuwa Serikali ilifanikiwa kuwafanyia
tohara wanaume hao kwa kutumia njia ya kuwaelimisha kwa kuwaelezea
umuhimu wa tohara na hatari inayowakabili kwa kuendelea kuishi bila
kufanyiwa tohara hasa kuambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwamo VVU.
Pia, taarifa hiyo inaeleza kuhusu mpango wa kuzuia
maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa mwaka 2005,
wajawazito 11,435 ambayo ni asilimia tisa ya wenye maambukizi ya virusi.
Inasema walipatiwa dawa za ARVs kuzuia maambukizi hayo kwenda kwa mtoto.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, wizara hiyo inaendelea
kutoa kupaumbele maeneo ya kudhibiti magonjwa ya ngono, utoaji ushauri
nasaha na huduma kwa wagonjwa wa nyumbani, elimu na habari, tiba na
matunzo, huduma ya maabara kwa wagonjwa waishio na VVU.
“Hamasa kwa Watanzania imekuwa ikiongezeka hasa
baada ya kampeni iliyoongozwa na Rais (Jakaya Kikwete) mwaka 2007, idadi
ya vituo vya upimaji iliongezeka kutoka vituo 521 mwaka 2005 hadi 2,200
mwaka jana,” inasema taarifa hiyo na kuongeza:
“Iidadi ya wananchi waliopatiwa huduma hiyo nayo
imeongezeka kutoka watu 365,189 mwaka 2005 hadi watu 17,008,475 Machi
mwaka jana.” ( R & Ed)
No comments:
Post a Comment