Matokeo ya mwanzoya
uchaguzi mkuu nchini Kenya yanaonyesha Uhuru Kenyatta akiwa anaongoza
kwa asilimia hamsini na nne dhidi ya Raila Odinga aliye na asilimia
arobaini na moja.
Ni uchaguzi ambao mamilioni ya wakenya
walishiriki kupiga kura licha ya visa vya vurugu kuripotiwa katika
baadhi ya sehemu za nchi ambapo takriban watu 15 wakiwemo polisi
waliuawa .
Wakenya walisubiri kwa zaidi ya saa
nane kupiga kura ikizingatiwa kuwa baadhi walikuwa katika vituo vya
kupigia kura mapema asubuhi saa za tisa na hata saa nane wakisubiri
vituo kufunguliwa.
Mamilioni ya wakenya wanatumai kuwa matokeo ya
uchaguzi huu yatawaunganisha wananchi hasa baada ya ghasia kushuhudiwa
baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Watu elfu moja na miambili waliuawa na
maelfu ya wengine kuachwa bila makao.
Matokeo ya mwanzo yanaonyesha Uhuru akiongoza kwa zaidi ya asilimia hamsini dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga, 68.
Tume ya uchaguzi inasema kuwa shughuli ya
kuhesabu kura huenda ikaendelea hadi Jumatano kwa sababu ya idadi kubwa
ya wapiga kura walioshiriki zoezi hilo.
Hatua hii nayo huenda ikachelewesha kutangaza matokeo rasmi ya uchaguzi mkuu.
Watu waliendesha shughuli hiyo kwa amani kwani
ndiyo ilikuwa kauli mbiu ya uchaguzi huu kwa hofu ya kutokea tena ghasia
za kikabila zilizoshuhudiwa mwaka 2007.
No comments:
Post a Comment