Matukio wakenya wakisubiri mshindi

Shughuli ya kuhesabu kura

Siku nne baada ya kupiga kura wakenya wangali kujua mshindi, wa urais, baadhi ya yaliyojitokeza hadi sasa ni pamoja na malalamishi ya muungano wa CORD wake Raila Odinga kutaka tume ya uchaguzi kusitisha shughuli ya kuhesabu kura wakidai kufanyika udanganyifu.

Leo mashirika ya kijamii yamekwenda mahakamani kuitaka mahakama kuu kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura

Nayo tume ya uchaguzi yasema idadi kubwa ya kura zilizoharibika ilitokana na hitilafu katika mtambo wake ambao ulikuwa unaongeza idadi ya kura hizo mara nane

Hadi kufikia sasa Uhuru Kenyatta ana kura 5,004,406 Raila Odinga ana kura 4,442,923

Wakenya wakiwa katika kipindi kigumu na cha wasiwasi kwani imechukua Tume ya Uchaguzi muda wa siku nne tangu kuanza shughuli ya kuhesabu kura na bado mshindi hajajulikana.

Kumekuwa na kila aina ya matukio katika muda huo wote. Tayari mashirika ya kijamii yameitaka mahakama kusitisha shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura inayofanywa na tume ya uchaguzi.Muungano wa CORD unaoongozwa na tume ya uchaguzi, umelalamika ukisema shughuli hiyo ina mizengwe na wanataka ianzishwe upya.

Tupe maoni yako kwenye ukurasa wetu wa Bofya Facebook kuhusu yanayojiri Kenya na tutauweka ujumbe wako kwenye mtandao wetu Bofya bbcswahili.com


15:40Dennis Tsunami Mbaka anasema kupitia Bofya facebook mataraiio ya wakenya ni mengi na licha ya kuzuka mambo mengi wakati huu wa uchaguzi hususan matokeo ya uchaguzi wa urais yakisubiriwa, anachotaka ni mchakato mzima kukamilika bila tashwishi na anaitakia nchi yake mustakabali mwema


15:32 Kuhusu kesi ambayo mashirika ya kijamii yameishtaki tume ya uchaguzi na kuitaka ikomeshe shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura za urais, ni mapema mno kwa hilo. Duru za kisheria zinasema kuwa kesi hiyo ina misingi duni kwani wanapaswa kusubiri matokeo rasmi ya uchaguzi kutangazwa ndiposa waende mahakamani


15:25 Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Isaack Hassan anatarajiwa kuhutubia waandishi wa habari wakati wowote kuanzia sasa

15:21Hanif Mohammed akiwa mjini Mombasa ameandika kwenye ukurasa Bofya facebook akizungumzia matokeo ya uchaguzi kwa sasa ya wagombea wakuu kuwa wanakanganywa na hesabu ya kura hizi ila anachoomba tu ni kuwepo amani


15:14 Sebastian Sabato kwenye ukurasa wa Bofya facebook anasema, ijapokuwa ninasubiri matokeo kwa hamu na gamu, kwa upande mwingine shughuli zangu zinaendelea kama kawaida.

No comments:

Post a Comment