Muda wa mwisho wa jeshi la Ufaransa Mali
Jeshi la Ufaransa limekuwa likisaidia majeshi ya Afrika kupambana na wapiganaji wa Mali kwa muda sasa
Rais wa
Ufaransa, Francois Hollande, amesema kuwa nchi yake itaanza kuondoa
wanajeshi wake kutoka Mali mwezi Ujao.
Aliongeza kuwa harakati za mwisho za jeshi dhidi ya wapiganaji wa Mali zitaendelea hadi mwishoni mwa Machi kufikia Aprili.
Bwana Hollande alisema kuwa harakati hizo zilipelekea kuuawa kwa viongozi wa wapiganaji, ingawa hakuwataja majina.
Mwanajeshi mmoja wa Ufaransa aliuawa pamoja na
wapiganaji 10 wakati wa makabiliano kati yao, kilomita miamoja Mashariki
mwa mji wa Gao.
Bwana Hollande alisema kuwa viongozi wa
wapiganaji wameangamizwa ingawa haijulikani ikiwa anazungumzia viongozi
wawili waliouawa wiki jana.
Nchi ya Chad, imesema kuwa wanajeshi wake,
waliokuwa wanasaidiana na wanajeshi wa Ufaransa, waliwaua makamanda
wawili wakuu wa wapiganaji,Abdelhamid Abou Zeid kutoka kundi la al-Qaeda
na kiongozi mkongwe wa wapiganaji wa kiisilamu Mokhtar Belmokhtar.
Wanajeshi wa Ufaransa hata hivyo bado hawajathibitisha taarifa hizo.
Takriban wanajeshi 4,000 wangali wako nchini Mali.
Wanajeshi wa Mali kwa ushirikiano na wanajeshi
wengine kutoka katika nchi kadhaa za Afrika, ikiwemo wanajeshi elfu
mbili kutoka Chad wamehusika na harakati hizo.
Ufaransa awali ilisema kuwa idadi ya wanajeshi
itaanza kupungua kuanzia mwezi Machi ikiwa mipango yote ingekwenda kama
ilivyopangwa.
No comments:
Post a Comment