Dar es Salaam. Dereva wa gari
lililomgonga na kumuua askari wa usalama barabarani, Elikiza Nko
(pichani) atafikishwa kortini wakati wowote baada ya upelelezi
kukamilika, ilielezwa jana.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani
nchini(trafiki), Mohammed Mpinga alisema hayo jana alipozungumzia tukio
hilo ambalo lilisababisha simanzi kwa watu wengi.
Mpinga alisema polisi walifanikiwa kumkamata
mhusika kwa mbinu za kipolisi na kwamba kwa jana alikuwa akihojiwa ili
kupata ushahidi utakaowezesha kumpeleka kortini.
Alisema dereva huyo ni kati ya wale wawili waliowakamata awali na hatimaye mmoja walimbaini kuwa ni mhusika .
‘’Juzi usiku tuliwahoji na mmoja wao
alitudanganya, tulipomuuliza dereva wa gari hili ni nani akajibu siyo
mimi nimeachiwa na mwenyewe amekimbia” alisema Kamanda Mpinga na
kuongeza kuwa baada ya kumbana alikiri kuwa ndiye.
Kwa mujibu wa Kamanda Mpinga marehemu ameacha mume
na watoto watatu. Maziko yanatarajiwa kufanyika leo katika makaburi ya
Mbweni yaliyopo Manispaa ya Kinondoni na yatahudhuriwa na viongozi
mbalimbali wa kitaifa.
Marehemu alifariki dunia baada ya kugongwa na gari
lililokurupuka kuufuata msafara wa Rais Jakaya Kikwete eneo la Bamaga
Mwenge jijini Dar es Salaam Jumatatu iliyopita alipokuwa katika ziara ya
kutembelea mkoa huo.
No comments:
Post a Comment