Mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema)
Mbunge wa Ubungo John Mnyika (Chadema), amewasilisha rufaa kwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi, dhidi ya agizo la Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Charles Kenyela, kuzuia mkutano wa hadhara ulioitishwa na mbunge huyo Machi 16, mwaka huu.
Katika taarifa yake jana, alisema aliwasilisha barua yenye kumbukumbu namba OMU\US\003\2013, ya kukata rufaa dhidi ya agizo la Kenyela ambalo limekiuka masharti ya kifungu cha 4 cha Sheria ya kinga, madaraka na haki za Bunge.
Mnyika alimtaka Waziri wa Mambo ya Ndani kurejea kifungu cha 43 (6) cha Sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma za Polisi wasaidizi, maelezo ya kutoridhika na amri ya kusimamisha mkutano iliyotolewa na kufanyiwa maamuzi.
Alisema Charles Kenyela alifanya makosa kwa kuzuia mkutano wa hadhara wa mbunge na wananchi wa bila sababu za msingi kinyume na matakwa ya Sheria ya Kinga, Madaraka na Haki za Bunge ambayo inaelekeza, mbunge anao uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara katika Jimbo lake na mamlaka zote zinazohusika zinawajibu wa kuwezesha mikutano hiyo kufanyika. Aliongeza kuwa, Kamanda Kenyela, aagizwe kugharamia mkutano mwingine wa Mbunge na wananchi kabla ya Aprili 9, 2013 ili kufidia gharama zilizotumika kwenye maandalizi ya mkutano aliouzuia.
CHANZO:
NIPASHE
No comments:
Post a Comment