Tume ya uchaguzi Kenya yakiri hitilafu za kimitambo
Tume ya uchaguzi imelaumiwa kwa kutokea hitilafu nyingi tu na mitambo yake
Tume huru ya
uchaguzi na mipaka nchini Kenya imekiri kuwa kulikuwa na hitilafu chungu
nzima za kimitambo, katika kutoa matangazo ya matokeo ya kura za urais
kutoka kwa vituo vya kupigia kura kote nchini.
Afisaa mkuu mtendaji wa tume hiyo,James Oswago
alielezea kuwa hitilafu hiyo ilisababishwa na kiasi kikubwa cha matokeo
yaliyokuwa yanapeperushwa moja kwa moja kutoka kwa vituo vya kupigia
kura kwa sababu ya ukosefu wa nafasi ya kutosha kwenye mitambo yake.
Akihutubia waandishi wa habari
katika ukumbi wa Bomas ambako matokeo ya urais yanatarajiwa kutangazwa,
Bwana oswago alisema kuwa tume hiyo iliweza kurekebisha mitambo yake.
Pia aliongeza kuwa maajenti wa wagombea wote wakuu wawili walifahamishwa kuhusu hutilafu hiyo.
Kugoma kwa muda kwa mitambo ya kupeperusha
matokeo, ilisababisha hali ya wasiwasi, baada ya IEBC kusitisha
kupeperusha matangazo kwa masaa kadhaa.
Maafisa wa Miungano yote ya Jubiliee na CORD,
walitetea kwa sababu ya kucheleweshwa kwa matokeo na kulaumu tume ya
IEBC, baada ya maafisa wake wote kuondoka katika ukumbi wa kutangazia
matokeo ya urais.
Kamishna mmoja mkuu wa tume hiyo aliwataka watu kuwa watulivu akisema hakuna sababu ya watu kuwa na wasiwasi.
No comments:
Post a Comment