Wen Jiabao afungua rasmi bunge China
Waziri mkuu mstaafu wa Uchina ,
Wen Jiabao, ameandaa sera za serikali ijayo kwa kipindi cha mwaka mmoja
ujao wakati alipofungua rasmi bunge la nchi , ikiwa ni awamu ya mwisho
ya kipindi cha ukabidhi wa mamlaka.
Bwana Wen amesema kuwa sera hizo zitatoa
kipaumbele katika kuhakikisha hali bora ya maisha ya watu kwa kuboresha
huduma za umma , kukabiliana na tatizo la uchafuzi mkubwa wa hali ya
hewa na kusafisaha serikali.
Matamshi yake hayo yanakwenda sambamba na ahadi
zilizotolewa na mkuu wa chama tawala cha kikomunisti , Xi Jinping, ya
kuinua viwango vya maisha ya raia na kumaliza ufisadi .
Bwana Wen alikuwa akihutubia wajumbe elfu tatu
wanaohudhuria kikao cha mwaka cha bunge la Uchina, ambacho
kimefunguliwa mjini Beijing.
No comments:
Post a Comment