Balozi Rehema Mabwai akifuta machozi wakati alipokuwa akilalamikia nyumba yake kuwa katika hatari ya kuvunjwa baada ya kuona ukuta wa uzio umejengwa kuzunguka nyumba yake.
Ivan Chibarangu akionyesha ukuta wa uzio uliojengwa na mafundi wanaodaiwa kulipwa na Kimbinyiko na baadae kuibomoa nyumba yake.
Mimea ya mahindi ikiwa imeanguka kwa kukanyagwa wakati wa ujenzi wa uzio uliozunguka nyumba tatu na wamiliki wake kutakiwa kuondoka na anayedaiwa kuwa mmliki wa mabasi ya Kimbinyiko
wananchi wa Kisasa West Blk A wakiwashangaa mafundi waliokuwa kwenye nyumba ya Ivan Chibarangu kwa ajili ya ujenzi wa uzio na kuboibomoa bila ulinzi wa polisi wala kibari cha mahakama.
MMILIKI wa mabasi ya Kimbinyiko adaiwa kuvamia nyumba za watu na kuzizungushia uzio, huku akiwatisha wenye nyumba, kuwadharirisha, kuzibomoa na kutumia polisi kuwasweka lupango wanapojaribu kudai haki zao.
Mmliki huyo wa Mabasi yaendayo mikoani yenye jina la kampuni ya Kimbinyiko bila ya Hofu yoyote aliamua kutekeleza adhima yake hiyo ya kuchimba msingi na kujenga uzio huo kwa siku mbili akizungushia nyumba 3 alizozikuta huku watu wakiishi ndani yake.
Jumapili hii Mmiliki wa nyumba mjawapo inayotazamana na Bwawa njiapanda ya Merriwa Manispaa ya Dodoma aliamua kujaza watu kwa kuamua kupiga Filimbi ili apate msaada kutokana na nyumba yake kubomolewa kwa kuvunjwa sehemu moja ya ukuta na Baadhi ya bati kung’olewa kwenye paa la juu.
Wakiongea kwa masikitiko wamiliki wa nyumba hizo Rehema Mabwai 58, Salome Mabwai 78, na Ivan Chibarangu walisema wanashangaa na kinachoendelea na hawajui cha kufanya maana mwenye pesa aliamua kuwatesa hivyo kutokana na unyonge wao bila kujali wao walifyeka na kujenga eneo hilo mwaka 1984 .
‘’Nimefika asubuhi nimekuta wamepanda juuu wanabomoa nyumba yangu nikapiga Filimbi ili nipate msaada baada ya watu kujaa wameacha lakini ona uhalibifu huu wa kubomoa sehemu ya ukuta na bati walizong’oa, leo sitoki maana nikitoka kufuatilia Sheria wenzangu wanajenga mpaka wamemaliza kuta za uzio’’, Alisema Chibarangu
Aidha Rehema Mabwai ambae pia ni Balozi na mmiliki wa nyumba ya pili aliongeza kuwa Kimbinyiko alimuahidi kumjengea nyumba ya vyumba viwili nje ya uzio atakapomaliza ujenzi wake na hivyo kuwataka wasiwe na wasiwasi
Alisema wao hawajui Sheria wala kujua pa kwenda kulalamika lakini wanaomba wasaidiwe ili wasiweze kupoteza haki zao kutokana na wao kuishi ene hilo kwa muda mrefu sawa amesema atanijengea mimi je mama ataenda wapi au nyumba yake haitambuliwi?
Kwa upande wake mmoja wa wapangaji 8 wa nyumba hiyo iliyoanza kubomolewa Valian kiona alisema wao ni wapangaji wa nyumba hiyo kwa kipindi cha miaka 3 na kwamba Ivan Chibarangu ndiye aliyewapangisha lakini wiki iliyopita alifika mtu ambaye hawakuwahi kumuona na kuwambia yeye ndiye mwenye nyumba hiyo.
‘’Jana Jumamosi alikuja tena wakati ujenzi wa uzio ukiendelea akatupa kila mpangaji 20,000 na kututaka tuhame kuanzia jana bila kujua ni wapi tunaenda labda Barabara ya Isiza au kule Bwawani na kila mtu akaondoka maana tuliogopa kupoteza vyombo vyetu kwa sababu alituambia ataibomoa leo’’, alisema
Kwa upande wake mmiliki huyo wa Mabasi ya Kimbinyiko alipotafutwa ili atoe ufafanuzi kuhusu tuhuma hizo alishindwa kupatikana pamoja na juhudi kubwa alizofanya mwandishi wa habari hizi aliyeshindwa kupewa ushirikiano na Fundi Juma Galan aliyewataka wananchi hao kutosema chochote kwa madai ya yeye kulipwa hivyo asizuiliwe kufanya kazi yake huku akikataa kusema lolote hata namba ya simu ya Bosi wake alikataa kutoa.
Hata hivyo ilibidi mwandishi atafute Moja ya Tiketi Za mabasi hayo na alipopiga moja ya namba ilipokelewa na mtu aliyejitamburisha kwa jina moja la Venus alipoelezwa alisema mkuu alikuwa polisi anshuhulikia swala hilo maana alienda na polisi kumkamata mmoja wa hao wenye nyumba.
Aliongeza kuwa angemjulisha bosi wake au kutuma namba yake ya simu ambayo hata hivyo haikutumwa na hata alipopigiwa tena alisema amuombe kibali cha kuitoa ndipo aitume lakini mpaka sasa haikutumwa wala kujibu meseji aliyotumiwa.
Kamanda wa polisi David Misime alipoulizwa kuhusu tukio hilo alisema Bado halijamfikia lakini atalifuatilia na kwamba atahusisha mamlaka zinazohusika ili zithibitishe nani ni mmliki halali wa eneo hilo ili Sheria itachukua mkondo wake.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment