Ajifungua mtoto kwa mshtuko

Sumbawanga. Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamke,  mkazi wa kitongoji cha Chemka ,Kata  ya Chanji Manispaa ya Sumbawanga mkoani Rukwa amejikuta akipata  uchungu  wa  ghafla na kujifungua   mtoto  wa kiume   chooni, nyumbani  kwake  kutokana  na mshtuko  alioupata  baada ya  kutolewa  kwa nguvu   katika  nyumba  hiyo  na dalali  wa mahakama.

Katika  tukio  hilo ambalo   mwanamke huyo (jina linahifadhiwa) alipata mshtuko  mkubwa  baada ya  dalali wa mahakama  kufika nyumbani  kwake  na kuanza  kutoa  nje vyombo vyake vyote  kwa madai kuwa nyumba hiyo  ilikuwa na mgogoro.

Kwa mujibu  wa  mwanamke huyo  baada ya dalali   kuwatoa  kwa nguvu  katika nyumba  hiyo  kwa  kutoa  nyombo  vyao vyote  nje  na kufunga  nyumba  hiyo  kwa makufuli  baada ya   kuhaha  na kukosa  sehemu ya kuhifadhi vyombo  hivyo  yeye  na familia yake  walilazimika  kulala  nje ya nyumba hiyo na kunyeshewa na mvua  usiku  kucha.

Alisema baada ya kutaabika  usiku kucha  kwa kunyeshewa na mvua  ilipofika  saa tano  asubuhi  alibanwa  na uchungu mkali  alipolazimika  kukimbilia  chooni  na kujifungua  mtoto  wa kiume akiwa hai.

No comments:

Post a Comment