Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (wa
tatu kushoto) akitoa maelekezo alipotembelea mradi wa ujenzi jengo la ofisi ya
mkuu wa mkoa Dodoma. Kulia ni Katibu Tawala Mkoa Dodoma Ndg. Rehema Madenge.
Mafundi wa kampuni ya China Railway Jiachang
Engeneering Ltd (CRJE Co. Ltd) inayojenga Jengo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma wakiendelea na kazi kama walivyokutwa na Katibu Mkuu Kiongozi (hayupo
pichani) mwishoni mwa wiki alipotembelea mradi huo.
Katibu
Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amewataka watumishi wa serikali kutambua kuwa
wanawajibu mkubwa wa kujenga taswira nzuri ya utumishi wa umma hapa nchini
kupitia utendaji uliotukuka.
Balozi
Sefue alieleza hayo mwishoni mwa wiki alipokutana na watumishi wa sekretarieti
ya Mkoa wa Dodoma ambapo alisisitiza kuwa watendaji na viongozi wote wa umma
kuanzia ngazi za chini za uongozi na utumishi wanatakiwa kuhakikisha wanatimiza
wajibu wao ipasavyo na kuondoa taswira mbaya inayouandama utumishi wa umma.
Katika
hatua nyingine baada ya katibu Mkuu Balozi Sefue kuona tatizo la ukosefu wa
ofisi kwa watumishi wa sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma na kutembelea mradi wa
ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma unaokwenda taratibu kutokana na
upatikanaji wa fedha, balozi Sefue amesema serikali inawajibu wa kuhakikisha
mradi huo unakamilika haraka iwezekanavyo.
Vilevile
ameahidi katika mwaka wa fedha ujao 2013/14 serikali inaweza kutoa mara mbili
ya fedha zilizoombwa na sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya uendelezaji
wa ujenzi wa mradi huo wa ofisi ambapo jumla ya shilingi bilioni tatu ziliombwa
kwa ajili ya kuendeleza ujenzi katika bajeti ya mwaka 2013/14.
Kwa
upande wake katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Ndg. Rehema Madenge alibainisha
kuwa pamoja na tatizo la ofisi ya Mkuu wa Mkoa kutokuwa na jrngo lake la ofisi,
matatizo mengine yanayoikabili sekretarieti ya Mkoa wa Dodoma ni pamoja na
Ufinyu wa bajeti kwa ajili ya miradi ya maendeleo na fedha kidogo za kuendeshea
ofisi wakati gharama za uendeshaji zinapanda.
Aidha
uchache wa watumishi hasa kwenye kada za afya ni tatizo linguine lenye kuhitaji
utatuzi na kumuomba katibu mkuu kiongozi kutoa vibali kwa maombi yote ya
kuajiri yatayomfikia mezani kwake na kuiomba serikali itenge bajeti ya kuajiori
watumishi wa kada zenye upungufu ili sekretarieti za Mikoa ziweze kuajiri na
kuziba nafasi wazi.
Akiwakilisha
watumishi wengine, Mwenyekiti wa TUGHE tawi la Hospitali ya Mkoa wa Dodoma Dr.
Lucy Mkandawile alisema kuwa matatizo mengine yanayogusa watumishi moja kwa
moja ni pamoja na uchelewaji kupanda vyeo, malimbikizo ya Mishahara baada ya
kupanda vyeo, malipo ya nauli za likizo na matibabu, fedha kwa ajili ya sare za
kazi, ufadhili wa masomo kwa watumishi kwa ajili ya kujiendeleza na mishahara
midogo.
Akijibu
hoja hizo katibu Mkuu alieleza kuwa serikali inazifahamu baadhi ya changamoto
zilizoelezwa na inazichukua zote pamoja na zile mpya zinazoendelea kuibuliwa na
kuahidi kuwa serikali itaongeza jitihada katika kuzishughulikia lengo likiwa
kuzidi kuboresha mazingira ya utumishi wa umma na hali za maisha za watumishi.
No comments:
Post a Comment