Wadau wa Mbeya wamelipongeza Jeshi la
Polisi Mkoani hapa kutokana na juhudi za kupambana na uhalifu hususani
kudhibiti mtandao wa majambazi sugu.
Wadau
hao walisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Diwani Athumani ndiye anayepaswa
kupongezwa kutokana na juhudi alizozionesha za kufichua mtandao wa majambazi
ikiwa ni pamoja na kuwakamata na kuwauwa wengine.
Akizungumza
kwa niaba ya wadau hao Nwaka Mwakisu ambaye pia ni Mjumbe wa Mkutano mkuu wa
CCM Taifa kupitia Umoja wa Vijana Mkoa wa Mbeya katika mkutano wa waandishi wa
Habari uliofanyika katika ofisi za Umoja wa Vijana CCM Mkoa wa Mbeya.
Mwakisu
alisema Historia ya Mkoa wa Mbeya ilikuwa Mbaya ambapo ilikuwa ikisifika kwa
matukio mabaya kama ya upigaji nondo, ubakaji, ushirikina na ujambazi ambavyo
vimeanza kutoweka kutokana na juhudi zilizooneshwa na Jeshi hilo kwa
kushirikiana na wananchi.
"
Kutokana na hali ilivyo sioni sababu ya kutompongeza RPC Diwani kutokana na
kupambana na uhalifu Mkoani Mbeya " alisema Mwakisu.
Alisema
kutokana na hali halisi ya Amani ya Mkoa wa Mbeya Wawekezaji watajitokeza kwa
wingi kufanya uwekezaji tofauti na ilivyokuwa ambapo wawekezaji walikuwa
wakikimbia Mkoa wa Mbeya kutokana na Vurugu zilizokuwepo.
Aliongoza
kuwa kutokana na juhudi za Jeshi la Polisi za kupambana na uhalifu alisema ni
vema kila Mwananchi akatambua mchango huo na kusaidia katika kuhakikisha kuwa
amani inaongezeka Mkoani Mbeya.
Mwakisu
alisema pamoja na kutokomeza uhalifu Mkoani hapa pia suala la kuwatumikisha
Vijana katika mambo yasiyokuwa na msingi wowote hususani kwenye vurugu ndiyo
sababu ya kuongezeka kwa uhalifu.
Alisema
taifa lolote duniani linalindwa na kuendelezwa na vijana hivyo alitoa wito kwa
wanasiasa kuacha kuwatumia vijana vibaya ambapo aliongeza kuwa Vijana wenyewe
wanatakiwa kujitambua na kujiunga kwenye vikundi mbali mbali ilikuepuka
kutumika kwa maslahi ya watu wengine.
|
No comments:
Post a Comment