Mbunge
wa jimbo la Singida mashariki Mh. Tundu Lissu akizungumza kwenye
uzinduzi wa kampeni ya nafasi ya udiwani kata ya Iseke tarafa ya Ihanja
wilaya ya Ikungi uliofanyika katika kijiji cha Iseke.
Baadhi
ya wananchi wa kijiji cha Iseke tarafa ya Ihanja waliohudhuria uzinduzi
wa kampeni ya udiwani kata ya Iseke uliofanywa na chama cha CHADEMA.
Baadhi
ya viongozi wa CHADEMA waliohudhuria uzinduzi wa kampeni ya udiwani wa
kata ya Iseke tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi.
(Picha zote na Nathaniel
Limu).
Na Nathaniel Limu.
Mgeni rasmi katika kampeni ya uzinduzi wa nafasi ya udiwani kata ya Iseke tarafa ya Ihanja wilaya ya Ikungi
Mh. Tundu Lissu, ameashindwa kuuza sera za CHADEMA na badala yake
ametumia muda na nguvu nyingi kuhimiza sera yake ya ‘katazo’ la wananchi
kuchangia maendeleo yao .
Mh.
Tundu Lissu ambaye ni mbunge wa jimbo la Singida Mashariki kupitia
tiketi ya CHADEMA, alipanda jukwaani huku akiwa mabeba makabrasha ya
michanganuo ya bajeti ya serikali ya kuanzia mwaka wa fedha wa 2010/2011
hadi 2013/2014.
Akisema
na kushangiliwa kwa nguvu na wananchi waliohudhuria uzinduzi huo
uliofanyika katika kijiji cha iseke, Mh Tundu Lissu aliweka wazi kuwa
“Mimi sitaki kabisa kuzungumzia habari za Amosi Mghenyi ambaye
ametusaliti kwa kuhama CHADEMA na kurejea CCM. Amosi kisiasa ni mfu,
kwa hiyo siwezi kupoteza muda wangu kuzungumiza mambo ya mfu”.
Amesema
ufunguzi wake utajikita zaidi katika kuwaelimisha wananchi wa kata ya
Iseke kwamba serikali inayo fedha nyingi na za kutosha kugharamia
maendeleo ya wananchi.
Akiijengea
nguvu hoja yake hiyo, amesema kwa mfano katika mwaka wa fedha wa
2010/2011, mkoa wa Singida, ulipewa zaidi ya shilingi milioni 903 za
undeshaji wa shule, lakini zilizotumika ni zaidi ya shilingi milioni 464
na kubaki zaidi ya shilingi 438.2.
Amesema
fedha hizo zaidi ya shilingi 438.2 zilizobaki, hazijaainishwa
zilipelekwa wapi. “Kwa vyo vyote zitakuwa zimeishia kwenye matumbo ya
mgambo na watendaji wa serikali ya CCM”.
Mh.
Tundu ambaye pia ni mwanasheria kitaaluma, amewataka wakazi wa kata ya
Iseke, kumchagua Emmnuel Jackson Jingu awe diwani wao, ili waondokane na
manyanyaso ya michango kama walivyojikomboa wakazi wa jimbo la Singida
Mashariki.
Wagombea
wengine wa nafasi ya udiwani kata ya Iseke ni Amosi Munghenyi wa CCM na
Abdallah Kinyenje maarufu kwa jina la Petro wa CUF.
No comments:
Post a Comment