Vikosi vya serikali Somalia
vimefanikiwa kuidhibiti upya ikulu ya rais katika mji mkuu Mogadishu
baada ya hapo awali wapiganaji wa kiislamu kuishambulia.
Maafisa wanasema washambuliaji wapatao watano kutoka kundi la al-Shabab - waliuawa walipoingia katika eneo la ikulu hiyo.
Washambuliaji hao wanadaiwa kulipua bomu lililotegwa kwenye gari karibu na langu kuu la Ikulu hiyo.
waziri wa habari wa Somalia Mustaf Dhuhulow
Waziri wa habari na mawasiliano wa Somalia
Mustaf Dhuhulow ameambia BBC kuwa tayari mmoja wa washambuliaji hao
amekamatwa na anahojiwa na polisi.
Waziri Mustaf amesema, '' Walishambulia ikulu ya
rais saa za jioni. Alikuwa watu washambuliaji watatu pamoja na dereva
wao. Washambuliaji hao waliuawa lakini dereva wao alipata majeraha
madogo na anazuiliwa na polisi na kuhojiwa. Walijaribu kuvamia Villa
Somalia lakini wakakomeshwa. Tutawapa maelezo zaidi baadaye. Na tutaweza
kutoa maelezo zaidi kwa raia wa Somalia na dunia nzima.''
Shambulio la Al shabaab Mogadishu
Hii ni mara ya pili kwa Al Shabaab kuvamia ikulu
ya rais mjini Mogadishu mwaka huu japo mara ya kwanza walifanikiwa
kuingia ndani.
Rais Hassan Sheikh Mohamoud hakuwepo wakati wa shambulio hilo.
Kundi la wapiganaji wa kiislamu Al shabaab
limefukuzwa kutoka mjini Mogadishu tangu mwaka wa 2011 lakini limekuwa
likifanya mashambulio ya kuvizia tangu wakati huo.
Wanamgambo hao wanaaminiwa kufanya mashambulio
kadhaa pia katika nchi jirani ya Somalia kama vile Kenya, Uganda na
Tanzania kama njia ya kulipiza kisasi kwa kuingia majeshi ya Umoja wa
Afrika nchini Somalia.
No comments:
Post a Comment