Mkurugenzi
wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA Dk Ally Simba amesema vifungu
vyote vilivyolalamikiwa na wadau kuhusu sheria ya makosa ya mtandao
vimefanyiwa marekebisho huku akiwataka wananchi hasa watumiaji wa
mitandao kujiandaa kuipokea sheria hiyo.
Rai hiyo imekuja zikiwa zimebaki siku chache kabla ya kuanza kwa
sheria hiyo ambayo inatarajiwa kuanza Septemba mosi mwaka huu ambapo
amesema kuanza kwa sheria hiyo kutasaidia mambo mengi sana ikiwemo
kulinda mifumo ya msingi ya tehama na kutolea mfano wa mitandao ya simu
za mkononi.
Kwa upande wake mtendaji mkuu wakala wa serikali mtandaoni Bw Jabri
Bakari kwa sasa serikali inajitihadi kushirikiana na wadau wa sekta
binafsi hasa wataalam wanaoshughulikia mifumo ya komputa kuhakikisha
wanakutana mara kwa mara kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu
wa suala la usalama wa mitandao.
No comments:
Post a Comment