Mwenyekiti
wa chama cha mapinduzi wa wilaya ya Sumbawanga mjini Bw Emmanuel
Selemani Kilindu, amechukua hatua ya kujiuzulu wadhifa wake huo kufuatia
kuhitilafiana kwa kiwango kikubwa na mbunge anayemaliza muhula wake, na
kudai kuwa licha ya kukabiliana na changamoto nyingi za kiutendaji
lakini pia anayaweka maisha yake kwenye hatari kubwa.
Akiongea na waandishi wa habari mjini Sumbawanga mbele ya baadhi ya
wanachama wa chama cha mapinduzi, mwenyekiti huyo wa CCM Bw Kilindu
amesema mbunge anayemaliza muhula wake katika jimbo la Sumbawanga mjini
Aeshi Hilal, amekuwa akikiuka kanuni nyingi za chama ikiwa ni pamoja na
kuwatumia wapambe wake kufanya vurugu hadi kufikia kutaka kuichoma moto ofisi ya chama hicho kwa maslahi yake, huku mwenyekiti wa jumuiya
ya wazazi ya wilaya hiyo Bw Michael Chifunda akimuunga mkono naye kwa
kuachia ngazi.
Kwa upande wao baadhi ya wanachama wa CCM wakiongea kuhusu sakata
hilo, wamesema chama sasa kimefikia mahali pabaya kwa watu kutumia fedha
zao kuwagawa wanachama na viongozi pia na kuwa kwenye makundi, hali
ambayo inaelekea kukidhoofisha chama hivi sasa.
No comments:
Post a Comment