Daktari bandia aliwaambukiza Ukimwi watu 100
Mwanaume mmoja aliyejidai kuwa daktari na kuwaambukiza watu zaidi ya mia moja virusi amefikishwa mahakamani nchini Cambodia.
Yamkini daktari huyo bandia alikuwa akiwadunga wagonjwa wake kwa sindano aliyokuwa ameitumia kwa mgonjwa aliyekuwa na virusi vya Ukimwi.
Yem Chhrin anakabiliwa na kosa la kuua na kuambukiza watu ugonjwa huo kwa kukusudia.
Aidha Bw Yem anashtakiwa kwa kuwalaghai watu kuwa ni daktari ilhali hana vyeti halali vya kuhudumia umma.
Iwapo atapatikana na hatia mahakama ya nchi hiyo huenda ikamhukumu kifungo cha maisha jela.
Waathiriwa walioambukizwa maradhi ya Ukimwi wanatokea katika kijiji cha Roka kilichoko Kaskazini Magharibi.
Mmoja wao ni kiongozi wa kidini wa madhehebu ya Buddha na mtoto wa miaka mitatu.
Takriban 10 kati ya waathiriwa hao wanakisiwa kuwa wameshakata roho.
Kwa mujibu wa ripoti za mahakama daktari huyo bandia amekiri kuhudumu bila vyeti maalum ila anakana kukusudia kuwaambukiza watu hao 100 virusi vinavyosababisha maradhi ya Ukimwi.
Assad afanya ziara ya ghafla Moscow
Rais wa Syria Bashar al-Assad amefanya mashauriano na Rais wa Urusi Vladimir Putin baada yake kufanya ziara ya kushtukiza Moscow.
Msemaji wa Rais wa Urusi Dmitry Peskov amesema Assad "alikuwa kwenye ziara ya kikazi Moscow" Jumanne na alifanya mazungumzo na Bw Putin.
Mwishoni mwa mwezi jana, ndege za kijeshi za Urusi zilianza kushambulia maeneo yanayodhibitiwa na wapinzani wa Assad nchini Syria.
Urusi imejitetea na kusema inashambulia tu makundi ya kigaidi na wapiganaji wa Islamic State.
Bw Peskov ameambia wanahabari kwamba viongozi hao wawili walijadiliana kuhusu viva hivyo alivyosema ni dhidi ya magaidi.
Aidha, walizungumzia kuendelea kwa mashambulio ya ndege za Urusi na mpango wa Syria kuhusu wanajeshi. Haijabainika iwapo Bw Assad bado yuko Moscow au amerejea Damascus.
Hiyo ndiyo ziara ya kwanza kabisa kufanywa na Bw Assad nje ya nchi tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria 2011, runinga ya serikali nchini Syria imesema.
Taarifa kuhusu mazungumzo hayo iliyotolewa na Kremlin inaonyesha Bw Putin akieleza Syria kama “rafiki” na kusema Urusi iko tayari kuchangia “sio tu kijeshi…bali pia katika mchakato wa kisiasa” kurejesha Amani nchini humo.
MHE. CHIKU GALLAWA AWATAKA VIONGOZI WA DINI KUSISITIZA AMANI NA UTULIVU WAKATI WA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 25
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa
akifungua Mkutano wa viongozi wa dini mkoani humo uliojadili masuala ya amani
na utulivu wakati wa uchaguzi Mkuu Oktoba
25
Viongozi wa dini waliohudhuria Mkutano
ulioitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mapema leo kujadili masuala ya amani na
utulivu wakati wa uchaguzi mkuu oktoba
25.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP David
Misime akifafanua jinsi jeshi la polisi Dodoma lilivyojipanga kusimamia amani
na utulivu wakati wa uchaguzi mkuu oktoba 25 mapema leo kwenye kikao cha
viongozi wa dini kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.
Subscribe to:
Posts (Atom)