1. Chris Cremence 100,000
2. Anonymous 500,000
3. Maggid Mjengwa 100,000
4. Raymond Kasoyaga 20,000
5.Edward Mgogo 10,000
6.Joachim Kiula 5,000
7.Libory Muhanga 5,000
8.Geofrey Kagaruki 10,000
9.Sadiki Mangesho 10,000
10. Edwin Namnauka 40,000
11.Daud Mbuba 10,000
12. Anonymous 200,000
13.Mikidadi Waziri 6,000
14. Bungaya Mayo 5,500
15. Abraham Siyovelwa 50,000
16. Godfrey Chongolo 22,222
17. Jacob Mwamwene 51,000
18. Dennis Bwimbo 153,683
Jumla:
1,298,000 ( Milioni
Moja Na Laki Mbili Na Tisini Na Nane Elfu Na Mia Tatu Na Themanini Na
Tatu)
Kiasi kilichobaki kutimiza lengo? 900,000 ( Kiasi cha shilingi lakini tisa)
Background:
Ndugu zangu,
Daud Mwangosi ambaye pia alikuwa ' Mwanakijiji' mwenzetu hapa Mjengwablog hatunaye tena.
Nimemfahamu
Daud Mwangosi tangu mwaka 2004 nilipofika Iringa. Tangu wakati huo,
amekuwa akiinipa ushirikiano mkubwa kwenye kazi ya kutangaza shughuli
za kijamii kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi. Ni kwa kupiga
picha za televisheni na kurusha habari kwenda Channel Ten; Iwe ni
kwenda naye Ilula au Njombe, Daud Mwangosi alikuwa tayari kila
nilipomwomba aongozane nami kwa shughuli ya kijamii.
Mara
nyingi nilimkuta Daud ofisini kwake ( Picha ya kwanza juu) akichapa
kazi na huku mkewe akimsaidia kazi nyingine. Daud Mwangosi alikuwa
mbunifu. Alikuwa ni mwenye kiu ya kujifunza mambo mapya kwenye
teknolojia ya habari na mawasiliano.
Najua
Daud Mwangosi alikuwa na malengo ya kuendeleza shughuli zake za
ujasiriamali. Mbali ya mambo mengine, alikuwa na Photocopy machine ya
kumwongezea kipato ambayo iliharibika mwaka jana. Akawa na ndoto ya
kuwa na studio ndogo ya kupiga picha za vipande ( Passport Size). Yote
ni katika kumwongezea kipato kutunza familia yake.
Leo
Daud Mwangosi hayuko nasi. Ameacha familia, mjane na watoto wanne;
Itika Mwangosi ( Mjane) Nehemia Mwangosi ( 17) Kidato cha Nne
Malangali Sekondari, Hetzgovina Mwangosi (12) Bathsheba Mwangosi (9)
na Moria Mwangosi ( 2)
Namini Daud Mwangosi angependa shughuli alizokuwa akizifanya ziendelee na zije kuwasaidia watoto wake pia.
Jana
na leo nimewasiliana na mjane wa marehemu Mwangosi ambaye bado yuko
Tukuyu. Nikamwambia kuna ' Wanakijiji ' wa Mjengwablog walioguswa na
msiba wa Mwangosi na wangependa kutoa pole yao imsaidie katika kupata
mwanzo kutoka hapa alipo sasa. Mjane wa Mwangosi amefarijika sana
kusikia habari hizo.
Kwa
vile tayari ameahidiwa msaada wa kusomeshewa watoto. Msaada
anaouhitaji kwa sasa ni kupata photocopy machine ( Used) na kodi ya
pango la ofisi. Jumla yake kwa yote hayo mawili haitazidi shilingi za
Kitanzania milioni mbili na laki mbili. Hivyo msaada anaouomba kwa
wenye mapenzi mema ni shilingi 2, 200,000 ( Shilingi milioni mbili na
laki mbili). Shughuli hizo zitamsaidia kujikimu.
Kutokana
na hali aliyo nayo sasa, Mwenyekiti wenu napendekeza nichukue jukumu
la kuratibu michango hiyo. Shime tushirikiane kufanikisha hili ili
tumsitiri mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi.
Napendekeza
ifikapo mwisho wa mwezi huu ( Septemba) tuwe tumefanikisha zoezi
hili kwa yeyote aliye nacho, hata kama ni shilingi elfu tano, ni
msaada mkubwa.
Mjengwablog
bado tuna rekodi nzuri katika kuchangishana kuwasaidia wenye
kuhitaji. Itakumbukwa, huko nyuma, kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya
michango ile ya watoto wa Somalia na kuikabidhi UNICEF, Dar es
Salaam. Ni zaidi ya shilingi milioni mbili.
Tulifanikisha mchango wa kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango, Madibira. Zaidi ya shilingi milioni nne.
Sasa ni zamu ya kumchangia mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Kinachohitajika ni milioni mbili na laki mbili.
Naam, kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.
Mwenyekiti wenu na familia yangu naanza kwa kuchangia shilingi laki moja.
Na kama kawaida, taarifa za waliochanga na kiasi kilichopatikana kitawekwa kwenye blogu kwa kila mmoja kuona.
Namna
ya kuwasilisha michango: Tumia M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au
NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa
walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid
Mjengwa)
Natanguliza Shukrani.
No comments:
Post a Comment