Financial
statement inayoonyesha kiwango anachodaiwa wakati fedha hizo
hazikulipwa na mwanafunzi huyu bado anadaiwa na chuo na kimeshikilia
vyeti vyake
Barua
ambayo chuo kiliandika kuonyesha kuwa fedha zilirudishwa bodi baada ya
kuwa hazikusainiwa na wanafunzi.na kuwa fedha ya mwaka wa pili
haikulipwa kabisa na bodi ya mikopo
Baada
ya kufuatilia suala lake,alilifikisha hadi wizara ya elimu,na wizara
ikawaandikia bodi kutaka kujua ukweli wa madai haya,Barua hii
haikujibiwa
Baada ya bodi kutojibu barua ya kwanza,wizara iliandika tena kuulizia suala hilo,Hadi sasa bado bodi haijajibu kitu.
Bodi
ya mikopo,inalalamikiwa kutafuna fedha za mwanafunzi MWESIGA CHRISTIAN
MICHAEL aliyehititimu DUCE mwaka 2011.Bodi inaonekana hawakulipa ada
yake ya mwaka wa kwanza na wa pili,bali walilipa ya mwaka wa tatu
pekee.Alipokuwa akifuatilia akiwa bado chuoni alikuwa akiambiwa hakuna
tatizo na ada zote zitalipwa.Bali amejikuta akidaiwa na chuo ada ya
miaka 2 zaidi ya milion 2 na chuo kimezuia vyeti vyake.Bodi ya mikopo
ambayo aliingia nayo mkataba sasa inasema haimtambui na bajeti yake
haipo tena.Hata hivyo uchunguzi wa mjengwablog umegundua kuna
udanganyifu kwa upande wa bodi kwani financial statement waliyotoa
inaonyesha amelipiwa ada.Isipokuwa mjengwablog,imegundua kuwa bodi,ama
watumishi wake walighushi kwa makusudi na kubadili majina ya mnufaika na
kulipa mtu hewa kwa miaka 2,ila wakalipa mtu stahiki mwaka wa tatu
pekee.Ajabu hata hivyo,Mwesiga Christian Michael,hakunufaika na fedha
hizo,bado anadaiwa na chuo na vyeti vyake vimezuiwa.Ajabu ni kuwa
inaonekana anadaiwa zaidi ya milioni 7 wakati hazikulipwa fedha hizo.
Ni wazi kuna udanganyifu na au wizi kwenye bodi ya mikopo,na
mjengwablog imeshindwa kujua ni vipi bodi imekaidi kujibu barua za
wizara mara mbili juu ya madai ya Mwesiga.Tunadhani wenye kuhusika
watafutwe na mamlaka husika ili wawajibike kwa wizi walioutenda.Hadi
sasa Mwesiga hajapata ajira kwa sababu hana vyeti vya shahada
No comments:
Post a Comment