Kanisa la Anglikana lataka kuwa na rais
Askofu Mkuu wa kanisa la
Anglikana, Rowan Williams, amefichua kuwa kanisa hilo linaandaa mpango
wa kumteua rais wa kanisa, ambaye atabeba sehemu ya jukumu la kuongoza
kanisa duniani.
Alisema mtu atayechukua nafasi hiyo ataweza
kusafiri kwa urahisi, na hivo kumuacha Askofu Mkuu kushughulika zaidi na
kuongoza kanisa.
Doctor Williams, ambaye anastaafu mwezi wa
Disemba baada ya uongozi wa miaka 10, alikiri kuwa hakuweza kufanya
mengi kuzuwia mgawanyiko kanisani juu ya swala la uhusiano wa jinsia
moja.
No comments:
Post a Comment