Kero na ghadhabu katika nchi za Kiarabu
Kumezuka ghasia zaidi nje ya ubalozi wa Marekani
mjini Cairo kati ya polisi na waandamanaji wanaokashifu filamu ambayo
wanasema kuwa inakejeli imani ya Kiislamu.
Runinga ya Misri ilionyesha gari likiteketezwa moto na watu wengine wakikimbia vitoza machozi.
Wakati huohuo maafisa wa Marekani
wanasema serikali ya nchi hiyo inachunguza ikiwa mashambulio ya jumanne
kwenye ubalozi wa Marekani katika mji wa Libya wa Benghazi yalikuwa ni
ya kupangwa au la .
Balozi wa Marekani nchini Libya , Christopher Stevens, aliuawa .
Maafisa wa Marekani wameelezea mashambulio hayo
kama yenye utata na yenye kupangwa kitaalamu na kuna tetesi kwamba
makundi ya jihad huenda yalihusika .
Awali ilifikiriwa kuwa mashambulio hayo yalikuwa
na uhusiano na maandamano ya kupinga filamu iliyokuwa inamkejeli Mtume
Mohammed.
Takriban waandamanaji mia mbili wamekusanyika
karibu na ubalozi wa Marekani mjini Cairo Misri kwa usiku wa pili
kuelezea hasira yao juu ya filamu hiyo .
Awali waandamanaji walirusha mawe kwenye ubalozi huo na vikosi vya usalama vikafyatua mabomu ya kutoa machozi kuwa tawanya.
Watu wenye silaha waliokuwa na maguruneti
walichomo moto jengo la ubalozi na walioshuhudia wanasema watu hao
walizingira eneo hilo.
Rais Obama amelaani vikali shambulio hilo na ameahidi kushirikiana na serikali ya Libya kuwafikisha mbele ya sheria wahusika
No comments:
Post a Comment