MICHAEL OWEN BADO YUPO YUPO LIGI KUU ENGLAND, FAHAMU ALIPOTOKEA NA MATATIZO ALIYOKUTANA NAYO HADI LEO ANATUA STOKE CITY

Michael Owen anatarajiwa kuanza kuichezea klabu yake mpya, Stoke mwishoni mwa wiki ijayo itakapomenyana na mabingwa Manchester City.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa kimataifa wa England, ambaye alitemwa na Man United mapema mwishoni mwa msimu, amejiunga na The Potters kwa mkataba wa mwaka mmoja kucheza Ligi Kuu na usajili wake umeidhinishwa.

Done deal: Michael Owen poses with his new Stoke City shirt after joining the club on a one-year deal
Michael Owen akiwa na jezi ya Stoke City baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja

Ligi Kuu ilisema mapema Jumatatu kwamba klabu hiyo imekamilisha orodha ya wachezaji 25 na wakati huo Stoke ilikuwa haijamuorodhesha mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 32. 

Inadhaniwa ameingizwa kwenye kikosi baada ya kuondolewa kiungo Michael Tonge.

Taarifa ya Ligi Kuu ilisema; "Bodi ya Ligi Kuu imeidhinisha Stoke City kumsajili Michael Owen. Hivyo, atakuwemo kwenye kikosi cha wachezaji 25 wa klabu hiyo kwa ajili ya Ligi Kuu".

Ready and waiting: Owen tweeted a picture of his boots lying idle on Monday
Owen ameweka kwenye tweeter picha za viatu hivi tangu Jumatatu
Glimpses: Owen was rarely able to shine for United though injury and bad form
Owen hakuweza kung'ara United kutokana na kuandamwa na majeruhi

WASIFU WA MICHAEL OWEN 

1996: Alisajiliwa na kikosi cha kwanza cha Liverpool akiwa na umri wa miaka 17 kutoka akademi ya klabu hiyo.
1997: Mei 6 - Aliifungia bao lake la kwanza klabu hiyo katika mechi na Wimbledon Uwanja wa Selhurst Park.
1998:  Alimaliza msimu akiwa mfungaji bora kwa kufungana na mwenzake katika Ligi Kuu, kwa mabao 18.
Mei 31 - Aliteuliwa kwenye kikosi cha Kombe la Dunia cha cha wachezaji 22 wa England.
Juni 22 - Alifunga bao akitokea benchi dhidi ya Romania, lakini England ikalala 2-1.
Juni 30 - Alifunga bao tamu sana dhidi ya Argentina kabla ya England kutolewa kwenye fainali hizo za Ufaransa 98 kwa penalti.
2001: Mei - Alifunga mabao mawili katika dakika saba za mwisho Liverpool ikitoka nyuma na kuifunga Arsenal 2-1 katika fainali ya Kombe la FA Uwanja wa Millennium.
Alicheza, lakini hakufunga wakati Liverpool inatwaa taji la tatu la msimu, walipoifunga Alaves kwa penalti 5-4 baada ya dakika 120 na kutwaa Kombe la UEFA.
September 1 - Mabao yake matatu (Hat-trick) yaliisaidia  England kupata ushindi mnono wa 5-1 dhidi ya Ujerumani katika mechi za kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia mjini Munich.
Desemba 17 - Alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Ulaya.
2003: Aprili 26 - Alifunga bao lake la 100 katika Ligi Kuu, likiwa la pili kati ya manne, katika ushindi wa 6-0 dhidi ya West Brom.
2004: Agosti 12 - Vyanzo vya karibu na Real Madrid vilisema klabu hiyo ya Hispania imekubali kuipa Liverpool pauni Milioni 38 na kuwapa mchezaji Antonio Nunez ili kumpata Owen.
Agosti 13 - Alifanyiwa vipimo vya afya na vigogo hao wa Hispania na kufuzu.
Michael Owen
2005: Mei 23 - Baada ya kufunga mabao 16 katika msimu wake wa kwanza Hispania, alielezea nia yake ya kubaki Real Madrid licha ya tetesi za kutakiwa na Newcastle.
Agosti 30 - Alisaini mkataba wa miaka minne na Newcastle, kwa dau la pauni Milioni 17.
Desemba 31 - Aliumia mifupa ya kwenye vidole vya mguu katika mechi waliyofungwa na Tottenham na kukaa nje ya Uwanja kwa miezi kadhaa.
2006: Machi 24 - Newcastle ilitangaza Owen anatakiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa wa mguu.
Juni 20 - Alipona na kupewa nafasi kwenye Kombe la Dunia, lakini aliumia goti katika dakika ya kwanza tu ya mechi ya kundi lao dhidi ya Sweden mjini Cologne na mara moja akatolewa. Alikaa nje ya Uwanja kwa miezi mingine tisa.
2009: Mei - Alimaliza msimu na mabao 10 huku Newcastle ikiipa mkono wa kwaheri Ligi Kuu katika siku ya mwisho.
Juni 22 - Ilithibitishwa hatasaini mkataba mpya na Newcastle.
Julai 1 - Akawa mchezaji huru baada ya mkataba wake na Newcastle kumalizika.
Julai 3 - Taarifa zilianza kumuhusisha na kuhamia Manchester United na baadaye akasaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa hao wa wakmati huo, baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Agosti - Aliichezea mechi ya kwanza ya ligi United, akitokea benchi dhidi ya Birmingham, kabla ya kufunga bao lake la kwanza kwenye mashindano dhidi ya Wigan siku sita baadaye.
Septemba 22 - Alifunga bao la ajabu na muhimu la ushindi katika dakika ya sita ya dakika za majeruhi kwenye ushindi wa 4-3 dhidi ya wapinzani wao, Manchester City.
2011: Mei - Alicheza mechi za kutosha msimu huo timu hiyo ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu, lakini alikaa benchi hadi mwisho wa fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Barcelona Uwanja wa Wembley, ambayo United ilifungwa.
Novemba 2 - Alitolewa mapema tu katika mechi ya makundi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Otelul Galati na kukosa msimu mzima uliobaki.
2012: Mei 17 - Aliandika kwenye Twitter kwamba Manchester United inaweza kumpa mkataba mpya baada ya kuwa na klabu hiyo kwa miaka mitatu.
Septemba 4 - Sasa akiwa huru amesaini Stoke mkataba wa mwaka mmoja na ameeidhinishwa na Bodi ya Ligi Kuu.

No comments:

Post a Comment