Na Riziki Bonzuma, Makete
Zaidi
ya wahitimu 120 wa utabibu na elimu ya kinywa na meno chuo cha Bulongwa
wametunukiwa vyeti na asikofu wa Dayosisi ya kusini kati Makete Revis
Sanga katika mahafari ya 2 yaliyofanyika chuono hapo.
Kabla
ya kukabidhi vyeti hivyo askofu Revis amewaasa wahitimu hao kuto
bweteteka na na elimu hiyo badala yake waendelee kusoma katika ngazi
zingine za elimu katika taluma hiyo askofu Revis pia amewaasa wahitimu
hao kuwa na moyo wa upendo kwa wagonjwa wawapo kazini.
Aidha
baada ya kupokea vyeti hivyo kulikuwa na kiapo kilichotolewa na matron
bi Ngwavi wa hospitali ya wilaya makete kwa niaaba ya mganga mkuu wa
wilaya makete kiapo huku mishumaa ikiwashwa kuashilia nuru upendo amani
na ukarimu .
Baada
haya kupokea vyeti niliongea na baadhi ya wahitimu ambao hakufisha
hisia zao kwani walionekana kufurahi na hatua walili ifikia huku
wakiupongeza uongozi wa chuo hicho kinanacho milikiwa kanisa la
kilutheri Tanzania dayosisi ya kusini kati Makete.
Penye mafanikio hapakosi changamoto kwani katika Risala iliyosomwa na
mkuu wa chuo hicho Dk Mcheshi amesema kuna changamoto kama uhaba wa
majengo na walimu pia suala la umeme pia limewakwamisha kufikia malengo
Kwani tangu march mwaka huu nishati hiyo nimewakwanisha kwani wamelazimika kutumia jenereta jambo ambalo linawaongezea gharama.
No comments:
Post a Comment