Afisa mmoja wa ubalozi wa
Marekani ameuawa na wengine wamejeruhiwa wakati kundi la watu
waliojihami na silaha walipovamia jengo hilo mjini Benghazi.
Maandamano pia yamefanyika mjini Cairo, Misri
Inaaminika kuwa watu hao walikuwa wanaandamana
kulaani filamu mmoja iliotengenezwa nchini Marekani ambayo wanasema
inamkejeli Mtume Mohammed.
Jengo hilo liliteketezwa kabisa na wandamanji hao waliokuwa na hasira.
Maandamano hayo yalichochea makabiliano kati ya
vikosi vya serikali na kundi la wanamgambo maarufu kama Ansar al Sharia
brigade, mjini Benghazi.
Msemaji wa serikali ya Marekani, amelaani
kitendo hicho na ameongeza kuwa wanashirikiana na idara ya usalama
nchini Libya kuimarisha usalama kwenye balozi zake.
Taarifa zinasema kuwa wakaazi wa mji mkuu
Tripoli, wamekuwa wakishawishiwa kupitia ujumbe kwenye tovuti za kijamii
wafanye maandamano lakini hakuna aliyejitokeza.
Sehemu ya filamu hiyo inasambazwa kupitia mtandao wa Youtube kwa lugha ya kiarabu.
Maandamano sawa na hayo pia yamefanyika mjini
Cairo nchini Misri. Kundi lingine la watu limeingia kwenye ubalozi wa
Marekani na kuteketeza bendera ya nchi hiyo.
Taarifa kutoka Cairo zinasema, maelfu ya
Waislamu na Wakristo wameungana kulaani filamu hiyo. Hata hivyo hakuna
aliyejeruhiwa kwenye maandamano hayo yaliofanyika Misri.
No comments:
Post a Comment