Majaji kususia kura ya maoni Misri


Wafuasi wa rais Morsi wakisherehekea mjini Cairo

Shirika linalowawakilisha mahakimu wa Misri limetangaza kuwa wanachama wake hawatoisimamia kura ya maoni ya rasimu ya katiba itakayofanyika wiki mbili zijazo.

Taarifa hiyo ya muungano huo wa mahakimu, inajiri baada ya kuwepo mvutano kati ya mahakama ya juu nchini Misri na wafuasi wa rais Morsi wenye itikadi kali za dini ya kiislamu.

Mahakama ya kikatiba imetangaza kuwa inasitisha shughuli zake kwa muda usiojulikana baada ya mahakimu wa mahakama hiyo kuzuiwa kutoa uamuzi kuhusu uhalali wa baraza rasimu hiyo ya katiba.

Upinzani unasema rasimu inashusha hadhi ya uhuru wa watu.

Makundi ya upinzani yaliitisha maandamano dhidi ya kura ya maoni juu ya katiba hiyo itakayofanyika siku ya Jumanne.

Walisema kuwa Rais Morsi alivunja ahadi ya kutoitisha kura ya maoni bila ya makubaliano ya wengi kuukubali wito huo.

"vuguvugu la National Salvation Front, linapinga kitendo kilichofanywa na ambachio hakikubaliki katu cha kuitisha kura ya maoni juu ya rasimu ya katiba ambayo imekataliwa na watu wengi''ilisema taarifa ya muungano wa vyama vaya upinzani kwa umma.

Upinzani unaamini kuwa rasimu hiyo inabana uhuru muhimu wa watu kikatiba.

No comments:

Post a Comment