Serikali ya Venezuela
inasema hali ya rais Hugo Chavez inazidi kuimarika baada ya kufanyiwa
upasuaji nchini Cuba Jumanne. Anaugua ugonjwa wa saratani.
Lakini mawaziri wamesema kwamba siku za usoni
zitakuwa ngumu kwake na itachukua muda mrefu kwake kupona. Waliwaonya
wananchi wa Venezuela wajitayarishe kwa siku za baadaye zenye hali
ngumu.
Chavez, mwenye umri wa miaka 58, sasa amefanyiwa upasuaji mara nne tangu alipoanza kuugua mwezi Juni 2011.
Taarifa kuhusu ni saratani ipi inayomsumbua Chavez haijawahi kutangazwa hadharani.
Maombi
Rais Rafael Correa wa Ecuador, mshirika wa
karibu wa Chavez, amesema ni sharti mifumo yake ya mabadiliko nchini
Venezuela iendelee, hata kama hataweza kurejea mamlakani.
Televisheni ya taifa ilirusha picha zilizoonyesha wananchi wa Venezuela wakimuombea rais kanisani.
Chavez angali nchini Cuba, na haijulikani ni
lini atarejea nchini. Anatarajiwa kuapishwa rasmi kwa muhula wake wa nne
kama rais katika kipindi cha mwezi mmoja ujao.
No comments:
Post a Comment