Bunge jipya lililokarabatiwa kwa zaidi ya dola milioni kumi
Wabunge nchini Kenya
wamejizawadia dola 107,000 kama marupurupu katika mojawpao ya vikao
vyao vya mwisho vya bunge hilo kabla ya uchaguzi mkuu kufayika mwezi
Machi.
Kila mbunge ataweza kupata mlinzi wa maisha,
pasi ya kidiplomasia na kupata huduma za juu zaidi katika viwanja vye
ndege kote duniani. Haya ndiyo mapendekezo yaliyo katika mswaada
waliopiitisha ukisubiri kuidhinishwa na rais Mwai Kibaki
Ni mara ya pili wabunge wamepitisha
mswaada huu wa kujizawadia mwishoni mwa vikao vyao vyabunge . Rais Mwai
Kibaki alitupilia mbali mswaada wa kwanza kama huu ambao ulizua ghadhabu
miongoni mwa wananchi.
Wabunge wa Kenya ni miongoni mwa wabunge
wanaopokea mishahara ya juu zaidi barani Afrika kila mmoja akipata dola
elfu kumi na tatu kila mwezi.
Lakini mshahara wa mkenya wa kawaida ni takriban dola 1,700 kila mwezi.
Mswaada huu, ulipitishwa siku ya Jumatano na
wabunge chini ya thelathini waliokuwa bungeni. Walikarabati bunge lao
kwa kutumia dola milioni kumi na mbili kulingana na stakabadhi za bunge
zilizotolewa hapo jana.
Malipo haya ni sawa na yale yaliyokuwepo katika
mswaada walioupitisha mwezi Oktoba, lakini wakati huu wabunge hao pia
wamependekeza marupurupu kwa rais ambaye atalipwa dola laki tatu sawa na
makamu wa rais na waziri mkuu.
Alipotupilia mbali mswaada wa kwanza , Rais
Kibaki lisema kuwa haiwezekani kwa wabunge kulipwa mamilioni ya dola
wakati uchumi ungali umedumaa.
Tume ya kushughulikia mishahara ya wafanyakazi wa umme, iliambia wakenya kuwa hakuna uhakika ikiwa hatua yao inakuika katiba.
Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu
yameelezea kukerwa sana na hatua ya wabunge. Tayari waziri mkuu Raila
Odinga amepinga mswaada huo akisema kuwa ni kama uhalifu dhidi ya
wakenya na kwamba anashauriana na rais Mwai Kibaki kuhusu hatua
itakayokuwa sawa kwa wakenya.
No comments:
Post a Comment