JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu 13, wakiwemo askari wawili wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na polisi mmoja kwa matukio ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha.

Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman akiwa na viongozi wenzake wa jeshi hilo la polisi wakati wa kuongea na waandishi wa habari wa Mbeya
Siraha zilizokamatwa na na jeshi hilo la polisi ndizo zilikokuwa zinatumika na majambazi hayo 
Moja ya bastora iliyotengenezwa kienyeji kwa kutumia vipande vya bomba lakini inatumia risasi za kawaida na nihatari sana siraha hii
Hizi ni vifaa vilivyokamatwa katika matukio mbalimbali yaliotokea mkoani hapa kamanda amewaomba wananchi wa mbeya kuja kuvitambua ofisini kwakwe 
Hizi ni siraha na sare za jeshi ambazo walikuwa wanatumia majambazi hao waliokamatwa kwa tuhuma za mauaji
Waandishi wa habari wakimsikiliza kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya
Mfanyabiashara maarufu wa eneo la Mwanjelwa, Gath Mbilinyi (32), anaetuhumiwa kuteka na kuua
Hawa ndiyo wanaotuhumiwa  kuwaua  dereva na utingo wake na kisha kwenda kuwazika porini  
Samahani kwa picha hizi zinasikitisha haya niamabaki ya miili ya tingo na dereva wake waliouwawa na watuhumiwa hapo juu


JESHI la Polisi Mkoa wa Mbeya, linawashikilia watu 13, wakiwemo askari wawili wa Jeshi la wananchi (JWTZ) na polisi mmoja  kwa matukio ya mauaji na unyang'anyi wa kutumia silaha.

Akizungumza na waandishi habari jijini Mbeya Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya  Diwani Athuman amesema watuhumiwa hao wamewagawanya katika makundi mawili, ambapo kundi la kwanza ni la watuhumiwa 9 wakiwemo askari hao wawili wakidaiwa kuhusika na tukio la kuwaua kikatili na kisha kuwazika dereva na utingo wake.

kundi la pili ni la watuhumiwa wanne wanaotuhumiwa kuhusika na mauaji ya dereva wa polisi lililotokea Wilayani Chunya mkoani hapa baada ya kufanyika uporaji wa shilingi milioni 2,200,000 katika kituo cha mafuta eneo la Matundasi wilayani chunya.

Akitoa ufafanuzi zaidi Kamanda Diwani amesema, katika tukio la kwanza ni lile lililotokea Februari 2 katika eneo la Mafinga,Mkoani Mbeya, ambapo watuhumiwa wa kundi la kwanza waliwateka dereva na utingo wake, Festo Kyando (45) na Jafari lililotokea na kuwaua kisha kwenda kuwazika porini.

Amesema dereva huyo alikuwa ametoka Jijini Dar es salaam kubeba mzigo wa wafanyabiashara kwa lengo la kuleta mkoani Mbeya, lakini kumbe walikuwa wakiwindwa na walipofika mkoani Iringa walitekwa na kufanyiwa mauaji hayo ya kinyama.

Kamanda Diwani amesema kufuatia tukio hilo jeshi la polisi lilianza uchunguzi mkali na hatimaye kunasa mtandao huo wa watu 9 wakiwemo askari hao wawili wa jeshi la polisi na JWTZ,ambao uchunguzi umebaini kuwa hutoa mavazi ya majeshi hayo na silaha.

Kamanda Diwani amewataja watuhumiwa hao kuwa MT.85393 Samwel Charles  Balumwina(31) wajiriwa wa jeshi la wananchi kikosi 844 kikosi cha Itende Mbeya na G.1901PC Samwel Kigunye (27) askari wa jeshi la polisi Jijini Mbeya.

Wengine ni mfanyabiashara maarufu wa eneo la Mwanjelwa, Gath Mbilinyi (32), Rajabu Mbilinyi(25), Gregory Mtega(25,Francis Sanga(30) pamoja na ndugu ambao ni wafanyabiashara maarufu katika mji wa Makambako mkoani Njombe ambao ni Japhet Ng'ang'ana(24), Claud Ng'ang'ana(36), Hilally Ng'ang'ana(30)

Hata hivyo amesema walifanikiwa kukamata bidhaa hizo katika eneo la Tunduma ambako tayari zilikuwa zimekamatwa na kwamba miongoni mwa watuhumiwa ndiye aliyeuziwa mzigo huo.

Amesema mali zilizookolewa katika matukio hayo kuwa ni Nondo 397 za aina tofauti pamoja na bando 18 za mifuko ya sandarusi(Sulphate) ambavyo vinashikiliwa na jeshi la Polisi Tunduma Wilani Mbozi Mkoani hapa.

Katika tukio la pili ni lile linalohusisha vifo vya watu wawili wilayani Chunya, ambao ni dereva wa polisi na dereva wa gari la majambazi baada ya kutokea kurushiana risasi.
Amesema tukio hilo lilitokea Februari 6 baada ya watuhumiwa wanne ambao wanashikiliwa na jeshi hilo kufanya uporaji wa shilingi milioni 2,200,000 katika kituo cha matundasi wilayani humo.
Amewataja madereva hao waliouwawa katika tukio hilo kuwa ni dereva wa polisi aliyefahamika kwa jina moja la Jafari, ambapo yule wa majambazi akitajwa kwa jina la  Shabani John.
Diwani amewataja watuhumiwa wanashikiliwa kwa tukio hilo kuwa ni Manase Kibona (37).Emmanuel Mndendemi na Masai Hongole, Mashaka George, John Mahenge, Narasco Mabiki.

Kamanda huyo amezitaja mali zilizookolewa katika matukio hayo kuwa ni Nondo 397 za aina tofauti pamoja na bando 18 za mifuko ya sandarusi(Sulphate) ambavyo vinashikiliwa na jeshi la Polisi Tunduma Wilani Momba  Mkoani Mbeya.

Aidha,kamanda Diwani  amevitaja baadhi ya vielelezo vilivyokamatwa  kuwa ni Bunduki aina ya Shot Gun moja ambayo namba zake zilifutika, Gobore moja ambalo pia namba zake zilifutika, Bastora tatu zilizotengenezwa kienyeji zisizo na namba na zinazotumia risasi za s/Gun.

Vingine ni Risasi 31 za Silaha ya SMG/SAR, Sare za Jeshi (JWTZ), suruali 4, mashati 4 kofia 3 na Viatu jozi mbili , Risasi 99 za S/GUN, Risasi 25 za Bastola na magari yenye namba T 464BLX TOYOTA COROLA,T381 BDR VITZ, T 251 AKU Toyota Pick Up ,T 193 BDY  Toyota Premio na T 214 ASV  Toyot Mark II.

Hata hivyo Kamanda wa Polisi anawashukuru wananchi wa Mkoa wa Mbeya waliojitokeza katika ktoa ushirikiano wa kuwasaka majambazi hayo ambapo pia anaendelea kutoa wito kwa watu wenye taarifa za watu ambao haeajakamatwa.
Ameongeza kuwa taratibu za upelelezi zimekamilika ambapo taratibu za kuwafikisha mahamakamani zinaendelea.

No comments:

Post a Comment