Katoliki waruhusu kuzuia mimba


KANISA Katoliki nchini Ujerumani limeamua kuhalalisha wanamke kutumia vidonge vya kuzuia mimba mara tu baada ya kubakwa.

Uamuzi huo umetolewa muda mfupi baada ya kutangaza kujiuzulu kwa Papa Benedict XVI mwanzoni mwa mwezi huu kwa sababu za kiafya.

Uamuzi huo umefanywa kutokana na mkutano wa viongozi wa Kanisa Katoliki nchini Ujerumani baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amebakwa kusema kuwa alizuiwa kufanyiwa matibabu siku mbili mfululizo katika Hospitali zinazofadhiliwa na Kanisa hilo kwa madai kuwa kuzuia mimba ni kinyume cha maongozi ya kanisa.

Maaskofu hao hatimaye walikubaliana kuwa itakuwa halali ikiwa vidonge hivyo vitatumiwa na mwanamke aliyebakwa.

kwa lengo la kuzuia kushika mimba badala ya kutoa mimba.

Hii ina maana kuwa itaweza kutumiwa tu kama kifaa cha kuzuia kushika mimba.

Vidonge hivyo hutumiwa na wanawake wengi wasiotaka kushika mimba baada ya tendo la ndoa.

Hata hivyo, Kanisa Katoliki nchini Ujerumani ambako Papa wa sasa alitoka, limegawanyika kufuatia tendo hilo la ubakaji.

Ubishi kama huo nchini Marekani haukufikia uamuzi baada ya pande zote zilizokuwa zikibishania dawa hiyo kusema kuwa ni vigumu kujua kama baada ya kitendo cha ndoa asubuhi inayofuata mwanamke ameshika mimba au la.

No comments:

Post a Comment