mtoto aungua, apofuka macho, fizi zaungua na meno kutoka.




 Mtoto Ombeni Mbeula akiwa amelazwa katika Hospital ya Rufaa ya General baada ya kuungua vibaya kutokana na kuangukia kwenye moto nyumbani kwao chitemo wilayani Mpwapwa Dodoma.

 Claudia Kigaila 27 akimuuguza mtoto wake Ombeni Mbeula 5 aliyeungua na moto mwezi wa 12 mwaka jana na kutelekezwa na Baba mzazi Julias Kigaila na ndugu wote baada ya kukata tamaa baada ya kufikili angekufa baaada ya muda mfipi.


Na John Banda, Dodoma

WAZAZI na ndugu wamtelekezea mama na Mtoto Ombeni Mbeula
wa umri wa miaka 5 alieungua moto na kusababishwa kuwa kipofu huku meno yakiporomoka kutokana na fidhi kuungua vibaya.

Tukio hilo l
ilitokea katika kijiji cha chitemo wilayani mpwapwa mkoani Dodoma Tarehe 10.12.2013 ambapo mama mzazi wa mtoto huyo Claudia Kigaila amalisema ametelekezewa na mume wake Julias Kigaila pamoja na ndugu wa pande zote mbili.

 Kigaila alisema wamemsusia ili aendelee kumtibu yeye kutokana na kun
g'ang'ania kumpeleka mtoto huyo hospital. wakati wao walitaka akawekwe nyumbani kwa sababu alikuwa ameungua sana hivyo hakukuwa na sababu ya kupoteza Gharama zao.

Amesema mtoto wake aliungua moto mwezi wa 12 mwaka 2012 baada ya kuangukia kwenye moto ambao ulikuwa jikoni baada ya yeye na kaka yake kukimbilia huko wakati mvua ilipokuwa ikinyesha na kuangusha ukuta huku kaka yake huyo wa miaka 7 akiangukiwa na udongo wakati yeye akiwa shamba.
''Hivi ni kweli mtoto wako mwenyewe ameungua kiasi hiki halafu ukamuweke nyumbani umuangalie tu hapana mimi ndiye niliyepata uchungu wa kumzaa nitapigana mpaka mwisho pamoja na mahangaiko yote haya mungu atanisaidia'', alisema

 Aidha Kigaila anasema  toka afike hospital hapo Tarehe 14. 12. 2012 mpaka sasa ndugu zake hao bado hawajafika kumuona wala kumsaidia chochote kiasi cha yeye na mtoto wake kulala na njaa ukiacha kukosekana kwa huduma ya matibabu kutokana na kukosa fedha.
Alisema kutokana na hali hiyo anawaomba wasamaria wema kuweza kumsaidia ili aweze kumuuguza mtoto wake ambaye kwa sasa macho hayaoni huku yakiwa na maumivu makali kiasi cha kutolala usiku kucha huku akiwa analishwa kwa kidole kutokana na mdomo kufunguka kwa shida.
''Naomba wenye uwezo wanisaidie kwa chochote ili niweze kumudu kumuuguza mwanangu maana sina jinsi ya kufanya kama hivi nimekuwa nikipewa msaada na ndugu wa wagonjwa wengine na wakisha ruhusiwa nabaki hivyo moyo una niuma sana kwasababu nina mume na ndugu lakini nateseka peke yangu'', alisema kwa uchungu
Claudia anasema kwa yoyote analiyeguswa na tukio hili anaweza kutoa msaada wowote na uatamfikia kupitia namba ya simu 

M. PESA 0757 498336 ya Ekiria Pascal wa Chinangali Dodoma ambaye amejitoa kumsaidia kwa hali na mali au unaweza kufika katika word ya watoto namba 14.
MWISHO

No comments:

Post a Comment