SHIRIKA la Maendeleo la Taifa (NDC) na Baraza la
Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), yametangaza kuunganisha
nguvu katika kukuwezesha wananchi, kupitia miradi inayoendeshwa na NDC.
Hatua hiyo inayoashiria Serikali kukunjua makucha dhidi ya migogoro baina ya wananchi na wawekezaji.
Katibu Mtendaji wa NEEC, Anaclet Kashuliza na
Mkurugenzi wa Viwanda vya Kuongeza Thamani wa NDC, Shanel Mvungi
walisema hatua hizo ni za awali kuwezesha wananchi.
“Tumeanza hatua
za awali za uwezeshaji wananchi kwenye maeneo jirani na mradi wa
uchimbaji Makaa ya Mawe ya Mchuchuma na Chuma Liganga, wilayani Ludewa,
tunaamini uwezo wao wa uchumi utakuzwa,” alisema Kashuliza.
Alisema utafiti wa awali umeonyesha kuwa yapo
mahitaji makubwa ya bidhaa mbalimbali, ambazo wananchi walio pembezoni
mwa eneo la mradi wanaweza kuanzisha.
Aliendelea kuwa wanaweza kuzalisha na kuuza na kunufaika wa ajira za moja kwa moja na kwamba, ajira hizo siyo chini ya 5,000.
Bidhaa hizo zilitajwa kuwa ni kuku, nyanya, vitunguu, matunda mbalimbali na mboga za majani.
Kashuliza alisema watendaji wa NEEC wamefanya
utafiti wa awali na kubaini jinsi wananchi wanavyoweza kunufaika.Alisema
wanajiandaa kutekeleza uondoaji vikwazo vilivyobainishwa ili wananchi
hao. Akizungumza kabla ya kukabidhiana mikataba hiyo, Mvungi alisema
baadhi ya wananchi wamekuwa wakinufaika na miradi inayowekezwa maeneo
yao.
“NEEC wameanzia kwenye mradi wetu wa Mchuchuma
na Liganga, wataendelea na mingine tutakayoanzisha, hali
itakayotofautisha miradi yetu na inayoendeshwa na wawekezaji wengine,”
alisema Mvungu.
Mvungi alisema mpango huo utalenga zaidi
kuwaelimisha wananchi wa maeneo jirani na miradi, kuona na kutumia fursa
zilizopo, ikiwamo kuwasaidia kukuza uwezo wa kubuni na kutekeleza
shughuli za uzalishaji.
No comments:
Post a Comment